Samsung ambao wameporomoka kutoka kwenye nafasi ya kwanza kwenye mauzo ya simu janja kwa mwaka 2020 wanaonekana kutoa rununu zenye mashiko kukimbizana na soko la ushindani wa kibiashara.
Tukiwa bado kwenye miezi ya awali kwa mwaka 2021 fahamu ya kuwa tayari Samsung wameshatoa simu janja mbili katika kipindi kifupi; rununu hizo ni Samsung Galaxy A32 4G na Samsung Galaxy A32 5G zikipishana mwezi na kidogo tangu kuzinduliwa kwao.
Sifa za Samsung Galaxy A32 4G
Kioo :
- Ukubwa: inchi 6.4
- Ubora: Gorilla Glass 5, AMOLED, ung’avu wa hali ya juu sana
Memori :
- Diski uhifadhi: 64GB/128GB
- RAM: 4GB
Kamera :
- Kamera Kuu: Megapixel 64, 8, 5 na 5
- Kamera ya Mbele: Megapixel 20
Betri/Chaji :
- Li-Ion 5000 mAh, uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
- USB-C
Kipuri mama :
- Helio G80
Programu Endeshi
- One UI 3.1, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeusi, Bluu na Udhurungi
- GB 64-$268 (zaidi ya Tsh. 616,400) na GB 128-$295 (zaidi ya Tsh. 678,500)
Mpangilio wa kamera za kwenye Samsung Galaxy A32 4G.
Sifa za Samsung Galaxy A32 5G
Kioo :
- Ukubwa: inchi 6.5
- Ubora:Â TFT LCD, 720p+
Memori :
- Diski uhifadhi: 64GB/128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
- RAM: 4GB, GB 6 na GB 8
Kamera :
- Kamera Kuu: Megapixel 48, 8, 5 na 5
- Kamera ya Mbele: Megapixel 13
Betri/Chaji :
- Li-Ion 5000 mAh, uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
- USB-C
Kipuri mama :
- Dimensity 720
Programu Endeshi
- One UI 3.1, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeusi, Nyeupe, Bluu na Udhurungi
- GB 64-$338 (zaidi ya Tsh. 777,400) na GB 128-$363 (zaidi ya Tsh. 834,900)
Samsung Galaxy A32 5G.
Teknolojia inazidi kuchanja mbuga; siku hizi simu janja za 5G zimekuwa si za kufanya watu kupigwa na butwaa kwani ziazidi kuzoeleka na wateja kuzipenda. Je, umevutiwa nazo kiasi cha kujipanga ili kuweza kuzinunua?
Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360
One Comment