fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Hii ndio nje ndani Samsung Galaxy A12

Hii ndio nje ndani Samsung Galaxy A12

Mwaka huu ukitaka kununua simu janja kutoka Samsung basi inaweza ikawa si jambo rahisi kusema kuchagua mara moja kwani zimetoka simu mbalimbali katika kipindi kifupi sana ikiwemo Samsung Galaxy A12.

Katika kupepesa macho yangu huku na kule nikakutana na simu hii ambayo ilitoka mwishoni mwa mwezi Disemba 2020. Kitu kizuri kuhusu simu hii ni kwa wale ambao tunapenda simu nzuri, bei ya kuhimilika basi Samsung Galaxy A12 inatufaa kwa sababu ya undani wa rununu yenyewe.

SOMA PIA  Bibi wa miaka 81 atengeneza app yake ya kwanza kwa ajili ya iOS

Sifa za Samsung Galaxy A12

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.5
 • Ubora: LCD, 720x1600px
Memori :
 • Diski uhifadhi: 64GB/128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
 • RAM: 3GB, 4GB na 6GB
Kamera :
 • Kamera Kuu: Megapixel 48, 5, 2, na 2
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 8
Kipuri mama :
 • Mediatek MT6765 Helio P35

Programu Endeshi

 • OneUI 2.5, Android 10
Rangi/Bei :
 • Bluu, Nyeusi, Nyeupe na Nyekundu
 • Bei inaanzia $174 (zaidi ya Tsh. 400,200)

  Galaxy A12

  Simu ya bei nafuu iliyowekwa betri lenye uwezo wa juu ili kuendana na nini ambacho soko linataka.

Kwa kuhitimisha tuu simu hii pia ina redio, teknolojia ya LTE lakini pia sehemu ya kuchomeka spika za masikioni bila kusahau teknolojia ya kutumia alama ya kidole.

Nini maoni yako kuhusu rurunu husika? Tupe maoni yako na usiache kutufuatilia kila inapoitwa leo kwa habari mpya zinazohusu teknolojia, sayansi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

SOMA PIA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

 1. […] Samsung A02s ambayo iliingia sokoni Jan 04 ya mwaka huu imekuwa ni simu ambayo inawalenga wateja ambao hawapendi mambo mengi yanayohusiana na rununu hivyo kuifanya kuwa simu janja ya bei nafuu. […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania