fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Uchambuzi

Samsung Galaxy M02s – Simu ya bei nafuu sokoni 2021 #Uchambuzi #Bei

Samsung Galaxy M02s – Simu ya bei nafuu sokoni 2021 #Uchambuzi #Bei

Spread the love

Simu ya Samsung Galaxy M02s imeanza kupatikana rasmi nchini India na inategemewa kuanza kupatikana katika mataifa mengine kote.

Simu hii ni simu yenye lengo la kukupatia kitu kizuri bila kuvunja akaunti yako ya benki.

Simu hiyo imeanza kupatikana nchini India kuanzia tarehe inategemewa kuanza kupatikana katika masoko mengine kama Afrika na bara la Ulaya kufikia mwezi wa Februari 2021.

Samsung Galaxy M02s

Samsung Galaxy M02s

Sifa na uwezo wa Samsung Galaxy S02s

Simu hii inakuja katika matoleo mawili

SOMA PIA  Xiaomi Kuachana Na Nembo Ya 'Mi' Katika Bidhaa Zake!

Toleo la  RAM ya GB 3 na diski ujazo wa GB 32, na jingine ni la RAM ya GB 4 na diski ujazo wa GB 64.

Samsung Galaxy M02s

Kwa ukubwa wa zaidi ya inchi 6 hii ni simu yenye display kubwa na nzuri kwa matumizi ya kuangalia video n.k

  • Programu endeshaji – Android 10
  • Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 450 na uwezo wa kusoma laini mbili za mawasiliano/simcard.
  • Kwenye rangi kuna nyeusi, bluu na nyekundu.
  • Simu zote zinakuja na uwezo wa kutumia memori kadi na zinasoma hadi microSD ya TB 1.
  • Display – Inaukubwa wa inchi 6.5, kioo cha teknolojia ya Infinity V display (Full HD)

Kamera

  • Inakamera tatu nyuma. Kuna kamera kuu ya megapixel 13, pamoja na kamera zingine 2 za ziada za megapixel 2 (Macro sensor & Depth sensor).
  • Kwa ajili ya selfi inakuja na kamera ya Megapixel 5
  • Betri – Betri ni la kudumu muda mrefu, likiwa ni la mAh 5,000. Pia simu inakuja na teknolojia ya kuchaji kwa haraka ya kiwango cha 15W

Simu ya Samsung Galaxy M02s : Uwezo wa kamera kutengeneza picha za aina ya ‘LIVE FOCUS’, kufanya mtu atokelezee zaidi ukilinganisha na muonekano wa mazingira yake

 

SOMA PIA  Kuchaji iPhone: Mmoja Afariki na Mwingine Hoi Hospitalini.

Bei: Bei rasmi kwenye tovuti ya Samsung inaweka toleo la GB 32 nchini India kwa bei ya takribani Tsh 300,000/= wakati toleo la GB 64 likiwa kwa bei ya takribani Tsh 320,000/=. Tunafuatilia vyanzo vya Tanzania kufahamu bei zake zitakapoanza kupatikana Tanzania.

SOMA PIA  Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge Kuanza Kupata Toleo la Android 6.0.1 Marshmallow

Je una mtazamo gani kuhusu simu hii? Je kuna unadhani kuna simu nyingine bora zaidi kwa bei hii?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania