fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huawei simu

2021 Huawei kutengeneza nusu ya idadi ya simu ukilinganisha na mwaka jana, Vikwazo vyawabana

2021 Huawei kutengeneza nusu ya idadi ya simu ukilinganisha na mwaka jana, Vikwazo vyawabana

Kwa mwaka 2021 Huawei kutengeneza nusu ya idadi ya simu ukilinganisha na idadi ya simu walizotengeneza kwa mwaka 2020. Hii imechangiwa na vikwazo vya Marekani.

Huawei duka simu

2021 Huawei kutengeneza nusu ya idadi ya simu ukilinganisha na mwaka jana, Vikwazo vya Kibiashara vyawabana

 

Katika taarifa ya Huawei kwa makampuni yanayosambaza vipuri kwake imesema kwa mwaka 2021 wanategemea kununua vipuri kwa ajili ya kutengeneza simu janja milioni 70-80, idadi hii ni chini kwa takribani asilimia 60 ukilinganisha na simu janja milioni 189 walizotengeneza na kuingiza sokoni mwaka 2020.

SOMA PIA  LG kuacha kutengeneza simu janja, gemu limekuwa gumu

Vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Huawei vimefanya hali iwe ngumu sana kwao kupata vipuri muhimu, hasa hasa vinavyohusisha mawasiliano ya 5G kwenye simu janja.

huawei honor

Kwa kuuza biashara nzima ya simu za Honor hili litakuwa ni pigo jingine litakalochangia kuporomoka kwa biashara hiyo

 

SOMA PIA  Fahamu kama simu zako zinafuatiliwa

Ingawa wameweka lengo la simu janja milioni 70-80 bado kuna wanaoona wanaweza shindwa fikia idadi hiyo, kuna wengi wanaoona idadi kamili inaweza ikawa simu janja milioni 50 – hasa hasa ukichukulia ya kwamba wameshauza pia biashara nzima ya simu zinazobeba jina la Honor.

SOMA PIA  Japan 'Kuishiwa' Namba Za Simu! :-)

Tayari data za mauzo ya simu kwa mwaka 2020 zimeonesha kuporomoka sana kwa nafasi ya Huawei katika ushindani dhidi ya Samsung, Apple na Xiaomi.

Tutegemee kwa 2021 Xiaomi na Oppo kuendelea kula soko la Huawei, kama mauzo yataendelea kuporomoka hivi tutegemee Huawei kushika namba tano kimauzo kwa mwaka 2021.

Chanzo: CNET na vyanzo mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania