Lionel Messi ni moja kati ya wachezaji bora kabisa na huawei wameona yeye ndio anafaa kuwawakilisha duniani. Ni kama Vodacom walivyofanya na Diamond Plutnumz tuu. Kwa kampuni lolote jambo hili huwa linaongeza mapato
Kampuni ya Huawei imesema kuwa imechagua nyota huyo kutokana na umahiri wake uwanjani na pia umaarufu wake duniani.
“Lionel Messi atasaidia bidhaa zetu kukonga nyoyo za watu hasa hasa barani Ulaya, Asia hata kwa walatino, ambapo Huawei wanaweka nguvu nyingi” – Alisema Kevin Ho, raisi wa Biashara ya simu za Huawei
Mara nyingi kampuni imekuwa ikizuia kuweka wazi kiasi gani inalipa katika madili yake makubwa lakini hili limewashangaza wengi baada ya kampuni hiyo kuweka wazi kuwa imemlipa mwanasoka huyo dola za kimarekani milioni 6.
Huawei inaona micheza kama ni sehemu ya uwanja mkubwa ambapo watu wanaweza wakabadilishana mambo mengi sana na kuboresha maisha yao zaidi. Kampuni imeliona hilo na kwa kumchagua Messi wanaona watabadilisha maisha ya watu wengi sana.
Kwa miaka kadhaa kampuni imekuwa ikiwekeza kwa wachezaji na timu mbalimbali za mpira, kama vile AC Milan, Atletico de Madrid, Arsenal, Sporting Cristal, Santa Fe, the America, Alexis Sanchez na Robert Lewandowski.
Huawei kwa sasa ni mmoja kati wa watengenezaji watatu wakuu wa simu janja ambazo zina soko sana duniani. Kampuni hasa linatikisa kwa simu zake zile za muendelezo wa Mate, P na G. Simu ya Huawei Mate 8 ambayo ilitolewa mwaka 2015 ambayo iliuza zaidi ya kopi milioni 3 duniani.
Huawei kwa sasa wanatarajiwa kuliteka soko kwa simu zao mpya za matoleo ya P9 (Huawei P9). Simu hizi zina sifa kedekede ikiwemo kuwa na kamera mbili za nyuma
One Comment
Comments are closed.