fbpx

Android, simu

Toleo jipya la Nokia 6 limetoka

toleo-jipya-la-nokia-6-limetoka

Sambaza

HMD Global wamedhamiria kabisa kuirudisha kwenye ramani ya ushindani wa kibiashara Nokia na tangu kununuliwa kutoka kwa mmiliki wake wa zamani, Nokia imekuwa ikirudisha heshima yake iliyokuwa nayo zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Nokia 6.1 ndio toleo jipya la simu janja iliyoka huku mtangulizi wake akiwa Nokia 6. Simu hii inaitwa kwa jina rahisi, “Nokia 6 4GB” sababu ikwa ni kuwa na RAM ya 4GB huku lile toleo lililopita ikiwa na RAM GB 3. Tofauti kati ya Nokia 6 na Nokia 6.1 ni kwenye RAM na diski uhifadhi tu.

Nokia 6 na 6.1 2018 zote zipo tayari kwa mauzo lakini na hiyo kufanya wapenzi wa simu za Nokia kuwa na wakati mzuri wa kuchagua simu ipi wanunue kati ya hizo mbili. Zifuatazo ni sifa za Nokia 6 2018 4GB:-

 >Ukubwa na ubora wa kioo. Toleo jipya la Nokia 6 kwa mwaka 2018 ina kioo chenye ukubwa wa inchi 5.5; ubora wa picha ukiwa ni 1080×1920 pixels na aina ya kioo ni IPS LCD. Kioo cha kwenye simu hii kinaonyesha picha katika kiwango cha ubora wa hali ya huu.

INAYOHUSIANA  BlackBerry Evolve na Evolve X zazinduliwa
Toleo jipya la Nokia 6
Zeiss wamekuwa wakitengeneza simu janja zao wenyewe lakini pia wakifanya kazi na makampuni mbalimbali kwenye upande wa kamera.

>Prosesa/Programu endeshaji. Hapa prosesa ni ile ambayo itakufanya ufurahie simu yako kwani itakuwa na kasi; prosesa ninayoizungumzia ni Octa-core Qualcomm Snapdragon 630 SoC kasi yake ikiwa ni 2.2GHz na programu endeshaji ni Android 8.1  Oreo lakini ikwa kwenye mpango wa kupokea sasisho la programu endeshi mpya ya Android One.

>Uwezo wa betri/Diski uhifadhi. Betri ya kwenye Nokia 6.1 ina 3000mAh (ambalo halitoki) kitu ambacho kinaifanya simu hii kuweza kukaa na chaji muda mrefu kutokana na kuw na nguvu kubwa pia ina teknolojia ya kuchaji haraka. Diski uhifadhi ni GB 32 au 64 lakini pia ikiwa na sehemu ya kuweka memori kadi ya mpaka GB 128.

INAYOHUSIANA  BlackBerry Passport: Kifahamu Kipya Kutoka BlackBerry

Sifa

Uwezo

 Kamera Kamera ya nyuma ina MP 16 ikiwa na flash mbili za LED, kamera ya mbele ina MP 8 na Zeiss ndio waliotengeneza kamera.
Usalama Ina teknolojia ya fingerprint iliyowekwa eneo la nyuma, inatumia kioo cha Gorilla 3
Laini za simu Inakubali laini 2
RAM Zipo zile zenye GB 3 na nyingine zina GB 4
Wembamba 148.8 x 75.8 x 8.2 mm (uzito ni gramu 172)
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni Ina ukubwa wa 3.5mm
Teknolojia nyinginezo GPS/ A-GPS, 3G HSPA, 4G LTE, Bluetooth 5.0, Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, USB Type C, ina ina redio
INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy S7 na S7 edge zaendelea kuangaliwa

Nokia 6.1 ya GB 3 za RAM+32GB ya diski uhifadhi ni $253|Tsh. 569,250 na ile yenye GB 4 za RAM pamoja na GB 64 za diski uhifadhi ni $282|Tsh. 634,500.

Vyanzo: The Indian Express, GSMArena, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Toleo jipya la Nokia 6 limetoka – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    May 10, 2018 at 8:45 pm

    […] post Toleo jipya la Nokia 6 limetoka appeared first on TeknoKona Teknolojia […]