fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huawei simu Uchambuzi

Ifahamu kiundani Huawei P40 4G

Ifahamu kiundani Huawei P40 4G

Spread the love

Katika ushindani wa kibiashara moja ya kampuni ambazo bidhaa zake zinapendwa Huawei Technologies Co. LTD ni miongoni mwao na wana simu janja nyingi, nzuri tuu sokoni.

Mwaka 2020 haukuwa mzuri kabisa kwa Huawei kutokana na sababu mbalimbali kiasi kwamba wakaporomoka kwenye ushindani. Huawei P40 ina karibu mwaka mmoja tangu itoke na sasa imeonekana kuwa ni wakati sahihi wa kuileta machoni pa watu toleo la 4G. Je, Huawei P40 4G ina sifa gani? Soma makala hii kuweza kufahamu undani wa simu janja husika.

SOMA PIA  Kaa Tayari,Baada Ya Nokia 9 Sasa Nokia 8 Ipo Njiani!

Sifa za Huawei P40 4G

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.1
 • Ubora: OLED, ung’avu wa hali ya juu sana
Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka GB 256
 • RAM: 8GB
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 3800 mAh, uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 22.5W
 • USB-C 3.1, OTG
Kipuri mama :
 • Kirin 990

Programu Endeshi

 • EMUI 10.1, Android 10
Rangi/Bei :
 • Bluu mpauko na Fedha
 • GB 128-$618 (zaidi ya Tsh. 1,421,400)
  Huawei P40

  Huawei P40 4G-teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa ndani ya kioo.

   

Simu janja hii imetoka Feb 26 na tayari imeshaingia sokoni. Je, toleo hili limekuvutia au unaona ni bora ubaki na hilo lililopita?

Vtanzo: GSMArena, Gizimochina

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

 1. […] wamehusika kwenye kamera za Huawei P40, Mate 20 Pro, P20 Pro, P30 Pro (2019) wakisifika katika kufanya muonekano wa picha uwezo wa kuvutia […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania