fbpx

Google, Maujanja, meseji, Teknolojia, Uchambuzi

Jinsi Ya Kufufua Barua Pepe Zilizofutika Katika Gmail!

jinsi-ya-kufufua-barua-pepe-zilizofutika-katika-gmail

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Kwa siku zinatumwa na kupokelewa barua pepe (E-mail) zaidi ya bilioni 205 kupitia mtandao wa Gmail. Namba hii kubwa ya barua pepe inapatikana kwa kuwa watu wamejiandikisha batika vitu mbalimbali kama vile mitandao tofauti tofauti kwa kutumia  barua pepe (Gmail) zao.

Kutokana na kuwa watu wanpokea barua pepe nyingi sana kwa siku, inakua ni vigumu sana kuzisoma zote na hata pia kuzipangilia. Saa zingine inawabidi kufuta barua pepe nyingi walizopokea kwa mkupuo, na pia inaweza tokea zile zenye umuhimu na zenyewe zikafutwa bila kusudio.Hili kama likikutokea leo Teknokona inakupa ufumbuzi.

 MUDA WA KUFUFUA

Kwanza kabisa jambo la muhimu kujua ni kwamba barua pepe zote zilizofutwa huwa zinakaa katika folda linasloitwa ‘Trash‘. Maisha ya barua pepe katika folda hilo ni siku 30 (mwezi) tuu. Baada ya hapo barua pepe hiyo itafutika moja kwa moja.Na baada ya hapo hautakuwa tena na uwezo wa kuweza kuifufua barua pepe hiyo.

INAYOHUSIANA  Jamaa Apigwa Faini Kwa Kosa La Kuendesha Huku Akitumia Saa Janja!

NJIA ZA KUFUFUA BARUA PEPE

  • Fungua akaunti ya Gmail kwa kutumia kompyuta
  • Ikishafunguka nenda katika kibox cha ku ‘search’ pale juu na kisha andika “in:trash” kisha bofya Enter.
Andika “in:trash” Katika Kibox Cha Kutafuta
  • Fungua barua pepe ambayo unataka kuifufua
  • Click‘ katika sehemu ya ‘Move To‘ na kisha chagua ‘Inbox
Nenda katika ‘Move To’ na kisha chagua ‘Inbox’

Mara tuu ukishamaliza fanya hivyo moja kwa moja barua pepe yako inatolea katika ‘trash‘ na kwenda moja kwa moja katika folda la ‘Inbox’

INAYOHUSIANA  Mpango wa Google kurejea Uchina

USHAURI KUTOKA TeknoKona.

TeknoKona inakushauri wewe mtumaji na mpokeaji wa barua pepe (hasa katika Gmail) kuwa badala ya kufuta (delete) barua pepe zako inabidi uziweke katika sehemu ya kumbukumbu (Archive) . Kama una barua pepe ambayo ni ya umuhimu basi haina budi kufanya hivyo kwa kumbuka endapo ukifuta barua pepe hiyo baada ya siku 30 itafutika moja kwa moja.

JINSI YA KUWEKA BARUA PEPE KATIKA ARCHIVE

  • Fungua akaunti ya Gmail
  • Fungua barua pepe unayotaka kuiweka katika kumbukumbu (Archive)
  • Angalia alama ya ‘Archive‘ na kisha ui ‘click‘ kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapo chini
INAYOHUSIANA  Kila County ya Kenya Kupata Darasa la Umeme-jua Ndani ya Boxi
Click Alama Ya ‘Archive’
  • Baada ya hapo barua pepe yako itahifadhiwa.

Hii ndio namna ya kupangilia barua pepe zako na kuhifadhi zile zenye umuhimu. zile ambazo hazina umuhimu unaweza ukazifuta lakini ikitokea umefuta zile zenye umuhimu kwa bahati mbaya unaweza fanya njia hiyo hapo juu.

Ni muhimu kutunza barua pepe wakati mwingine zinakuwa ni ushahidi tosha juu ya jambo fulani (Mfano katika makubaliano).

Fuata njia hizi uwe mtaalamu, kama ukikwama usisite kutuandikia katika sehemu ya comment hapo chini. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*