Kama wewe ni mtumiaji wa tovuti za manunuzi na taarifa muhimu za nchini basi utakuwa umefahamu ya kwamba kwa sasa ukitembelea tovuti ya ZoomTanzania utarushwa kupelekwa kwenye tovuti ya Kupatana.com.
ZoomTanzania.com ni moja ya tovuti ya miaka mingi zaidi Tanzania. Ni tovuti iliyokuwa inamuwezesha mtembeleaji kupata taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa mbalimbali, zinazouzwa na watu binafsi au makampuni. Ilikuwa sehemu nzuri ya kupata bidhaa zilizotumika na taarifa za ukodishaji nyumba na huduma zingine mbalimbali.

Tovuti ya ZoomTanzania.com imekuwepo tokea mwaka 2009. Kwa muda mrefu tovuti hiyo ilishakuwa kwenye orodha ya tovuti zinazotembelewa zaidi nchini.
Changamoto kwa tovuti za mauzo
Mtandao wa Instagram umeleta changamoto kubwa kwa tovuti za mauzo ya bidhaa, mpya au zilizotumika. Kwa sasa wauzaji wengi pamoja na wateja wanaamini hawaitaji kutembelea tovuti ili kupata taarifa muhimu za bidhaa na ulinganishaji wa bei. Wengi wanaenda moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kutafuta huko. Suala hili limeathiri sana mitandao iliyokuwa inategemea udalali kama sehemu ya mfumo muhimu wa biashara yake (kupata watumiaji wa tovuti).
No Comment! Be the first one.