fbpx

Teknolojia

Uwezo wa kuwagawa washiriki kwenye makundi ndani ya Google Meet

kuwagawa-washiriki-kwenye-makundi-ndani-ya-google-meet

Sambaza

Biashara ni ushindani na siku hizi watu hawategemei tena Skype peke yake ili kuweza kufanya mawasiliano na watu kwa njia ya maandishi au picha mnato bali kuna WhatsApp, Zoom, Google Meet, n.k.

Katika kipindi cha miezi ya karibuni Google wamekuwa wakiboresha bidhaa yao-Google Meet katika jitihada za kuendana na kasi ya washindani wake na hata kuvutia watu wengi katika kipindi hiki ambacho inawalazimu watu kuonana kwa njia ya mtandao.

Google wameamua kufanya majaribio ya kipengele cha kuweza kugawanya watu kwenye makundi mia moja kupitia wateja wanaotumia G Suite Enterprise for Education ambapo walimu/wana taaluma wanaweza kuwagawanya washiriki wao mara 100 na wote wakaweza kuwasiliana kwa wakati mmoja; mpangilio wamakundi hayo unafanywa na Google wenyewe bila kufuata mtiririko ingawa mwalimu anao uwezo wa kurudi nyuma na kuongeza au kupunguza idadi ya washikiriki kwenye kundi lolote kadri ambavyo itakuwa inafaa ingawa ukomo wa kugawanya watu kwenye makundi ni 100 tu.

INAYOHUSIANA  Waiba Tsh Bilioni 27.9 katika zaidi ya ATM 1,400 ndani ya masaa 3!
washiriki
Google waamua kuanza G Suite Enterprise for Education katika kuwezesha kugawa watu katika makundi.

Kipengele hiki si kipya kwa yule anyetumia Zoom kwani kimekuwepo tangu mwaka 2015 ingawa huko inawezekana kugawanya washiriki mara 50 na katika jitihada za kujitofautisha Google Meet imefanya kitu kilekile lakini kwa hatua moja zaidi.

Hapana shaka kuwa katika siku za usoni kipengele hicho cha kuweza kuwagawa washiriki kwenye makundi kitaweza kupatikana kwa watumiaji wote wa Google Meet lakini kwa sasa inatubidi tuwe na subira ya kusubiri vitu vizuri.

Vyanzo: 9to5Google, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*