Je, iPhone ni simu zisizoweza kudukuliwa? Wengi wamekuwa wakiamini hivyo ila kutana na programu ya Karma, programu hii inasemekana inazama ndani ya simu za iPhone kwa urahisi sana.
Skendo ya kuabisha imeripotiwa na chombo cha habari cha Reuters, katika taarufa hiyo inasemekana serikali ya shirikisho la Falme za Kiarabu (UAE – United Arab Emirates).

Kupitia programu ya Karma shirikisho hilo limekuwa likidukua na hivyo kufuatilia mambo mbalimbali ya watu wakubwa tuu kama vile Mfalme wa Qatar, Makamu Waziri Mkuu wa Uturuki mstaafu na wengine wengi – ikiwa ni pamoja na raia wa Marekani kadhaa.
Je, mfumo wa Karma unafanyaje kazi?
> Mfumo wa Karma haunahitaji ujuzi mwingi kwa mtu anayeutumia, kinachoitajika ni akaunti ya Apple ID au namba ya simu inayotumika kwenye iPhone husika.
> Baada ya hapo mfumo wa Karma unatuma ujumbe wa katika mfumo wa iMessage, ujumbe huo ukifika tuu kwenye simu husika basi moja kwa moja njia ya mawasiliano kati ya programu hiyo na iPhone husika inakuwa imekamilishwa, tena bila mwenye simu kutambua.

Programu ya Karma unaweza kuiba data mbalimbali kama vile picha, video, nywila (nenosiri), ujumbe na data zingine za apps zilizo kwenye iPhone husika.
Wafanyakazi katika mradi uliokuwa ukifahamika kama Raven ikisimamia kazi hii wengi wao walikuwa tayari walishawahi kufanya kazi katika shirika ya kiusalama na kijasusi Marekani (NSA).
Inadaiwa shirikisho la Falme za Kiarabu (UAE) zilitumia teknolojia hata dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu. Apple hawajatoa taarifa yoyote kuhusu habari hii, na vyanzo vya habari vinauhakika hadi mwisho wa mwaka 2017 bado programu ya Karma ilikuwa inaweza kuingia kwenye iPhone yoyote kwa urahisi.

Hii skendo bado ni mpya kabisa na tutegemee kuona shirikisho la Falme za Kiarabu likipata lawama kali kutokana na jambo hili, Marekani ni mshirika wa karibu sana wa serikali ya kifalme ya UAE na itakuwa vigumu kuamini ya kwamba hawakuwa wanafahamu kuhusu uwepo wa mradi wa Raven.
Vyanzo: Reuters na vingine mbalimbali