fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Kampuni ya Google Yafanya Mabadiliko ya Logo

Kampuni ya Google Yafanya Mabadiliko ya Logo

Spread the love

Baada ya mabadiliko makubwa kufanyika kwa kampuni ya Google, hii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa kampuni mama itambulikayo kwa jina la ALPHABET Google waamua kufanya mabadiliko katika logo yao.

Muonekano wa logo mpya

Muonekano wa logo mpya

Logo mpya yenye muonekano nyororo zaidi wamedai ni nzuri na bora zaidi ata kwenye vifaa kama vile simu, ‘eti’ inafunguka haraka zaidi bila kutumia data nyingi.

Logo ya zamani juu, mpya chini

Logo ya zamani juu, mpya chini

Ingawa kwa wengine wanaweza kuona ni mabadiliko machache tuu kwa logo ya kampuni hiyo kiuhalisia ni kwamba kuna mabadiliko mengi ya kiundani zaidi yanaendelea katika kampuni hiyo. Na tunaamini mabadiliko haya ya logo ni moja kati ya mabadiliko mengi yanayoendelea katika kampuni hiyo sambamba na uwepo wa kampuni mpya ya ALPHABET.

Kushoto logo ya zamani na kulia ni mpya itakayokuwa inawakilisha ile ndefu

Kushoto logo ya zamani na kulia ni mpya itakayokuwa inawakilisha ile ndefu

Je kati ya logo hii mpya na ile ya zamani ni ipi umeikubali zaidi?

SOMA PIA  TV kwenye chumba cha mtoto/watoto wako humsababishia kuongezeka uzito #Utafiti
Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania