Vita katika apps za kuchati zinazidi kupamba moto. Instagram nayo yaleta mambo mapya yanayozidi kuifanya ishindane moja kwa moja na apps zingine kama vile Snapchat. Kila apps iliyo kwenye simu janja zetu inataka tutumie muda mwingi zaidi kwake kuliko kwenye apps zingine.
Snapchat ni app ya kuchati ya iOS na Android ambayo inakua kwa kasi sana kwa sasa. Inawatumiaji zaidi ya milioni 100 na sifa zake kubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa mtu mmoja mmoja kutumiana picha zenye maneno n.k na ujumbe huo kufutika baada ya muda mfupi wa kusomwa.
Instagram kupitia sasisho (update) mpya wameleta mambo mapya katika app yao ya takribani watumiaji milioni 300.
- Tuma ujumbe wa picha au video kwa mtu mmoja au kundi upendalo
- Uwezo wa kuchati na mtu mmoja au katika kundi flani tuu, hii ni pamoja na uwezo wa kutumia maneno tuu bila picha
Mwanzo unapoweka kitu Instagram kilikuwa kinaonekana kwa watu wote wanaokufuatilia katika huduma hiyo, kuanzia sasa utaweza kuweka picha na kuwaonesha watu kadhaa tuu badala ya wote wote. Mazungumzo yenu yote mtakayofanya chini ya picha au video hiyo ni nyie tuu ndio mtaweza kuyaona.
Instagram wanaamini kufanya hivi kutawawezesha watumiaji wao wengi kutumia muda mwingi zaidi ndani ya app yao na kupunguza kufanya mazungumzo mengine ya namna hiyo kwenye apps nyingine kama vile Snapchat.
Inasemekana kwa sasa vijana wengi wanapendelea kufanya mazungumzo mengi kupitia njia za kutumiana picha katika apps kama vile WhatsApp, Instagram na Snapchat. Kwa uamuzi huu Instagram wanatemea kuweza kuwavutia watu wengi zaidi ambao vinginevyo wangekuwa wanafanya mazungumzo yao katika apps kama Snapchat.
Je una maoni gani na mpya hii? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja Tanzania kwa habari na maujanja ya kiteknolojia.
Bofya Kupakua;
[socialpoll id=”2292414″]
No Comment! Be the first one.