Kama umechoka tumia mtandao wa kijamii wa facebook au hata kama unataka kubadilisha ukurasa huo huna budi kuufuta. Achana na kusitisha kwa mda (Deactivate), nazungumzia kuufuta kabisa katika mtandao wa facebook.
Hii inamaanisha baada ya kufuta ukurasa huo hakuna mtu yeyote anaeweza kuuona na hiyo ina maana hata wewe huwezi kuuona tena. wengi wetu njia hii hatuifahamu, sisi tunajua tuu ile ya ku ‘deactivate’ ambayo tunafanyaga na baada ya muda tukijisikia kurudi facebook, tunaweza fanya hivyo kwa ku ‘log in’ tena katika akaunti zetu
Leo TeknoKona inakufundisha maujanja (Mapya kwako) kuhusu jinsi ambavyo unaweza kufuta akaunti yako ya facebook kwa muda na jinsi ambavyo unaweza futa moja kwa moja
JINSI YA KUSITISHA KWA MUDA (DEACTIVATE)
Ngoja kwanza tuangalie namna ya kusitisha akaunti zetu za facebook kwa muda ili kama tukitaka tuendelee kuzitumia tuweze fanya hivyo pia.Zifuatazo ni njia za kuwezesha hivyo:
- Fungua akaunti yako ya facebook
- Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
- Baada ya hapo ‘click’ Settings
- Ukiwa katika Settings katika upande wa kushoto utaona Security bofya hapo
- Sasa chagua “Deactivate Your Account” katika machaguo yaliyojitokeza
JINSI YA KUIPATA AKAUNTI ULIYOISITISHA KWA MDA (DEACTIVATE)
Hii ni raahisi kabisa —wewe unahisi itakua ni vipi? haha!— hapa hakuhitaji jasho kabisa. Ingia facebook alafu ‘log in’ kwa kutumia taarifa zako ulizokuwa unazitumia kama kawaida. Moja kwa moja itafunguka akaunti yako. Endelea kufurahia kutumia facebook
JINSI YA KUFUTA AKAUNTI YA FACEBOOK MOJA KWA MOJA
Kama umeamua kuwa hutaweza endelea tumia akaunti yako ya facebook au mitandao ya kijamii imekuchosha (ndio! mitandao inaweza ikakuchosha saa zingine). Ikitokea hivyo unaweza kuwaza kufuta ukurasa wako moja kwa moja sio? Njia hii haijulikani kwa watu wengi lakini asante kwa TeknoKona na wewe utakuwa fundi ndani ya mda mchache
Kabla ya yote inashauriwa mtu kushusha (download) nakala ya taarifa zako za facebook
Kufanya Hivyo, Fuata Njia Hizi
- Fungua akaunti yako ya facebook
- Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
- Kisha ‘click’ katika settiings
- Katika “General” chagua “Download a copy of your Facebook data.” kwa ku’click’ hapo
- Baada ya hapo bofya katika hii link https://www.facebook.com/help/delete_account na kisha nenda kwenye ‘Delete My Account’
Baada ya hapo utakuwa umefuta akaunti yako ya facebook moja kwa moja. Hii inamaanisha kuwa hutaweza kuitumia akaunti hiyo kamwe maana hii ni tofauti na kusitisha kwa mda (deactivate)
One Comment