fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Maujanja Mtandao wa Kijamii Teknolojia YouTube

Jinsi ya kutengeneza Youtube Channel

Jinsi ya kutengeneza Youtube Channel
Spread the love

Moja kati ya njia za kujiingizia kipato kupitia mtandao ni kwa kutengeneza Youtube Channel . Kampuni ya Google kupitia huduma yake ya Youtube ya kuangalia video mtandaoni imewapa nafasi watumiaji wenye Youtube Channel kujiingizia kipato kupitia matangazo mbalimbali yatakayokuwa yanaonyeshwa katika video wanazotuma pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wafuasi waliojisajili katika channel yako.

Kuna hatua mbalimbali unazohitaji kufuata ili uweze kutengeneza Youtube Channel ila kigezo cha kwanza cha kuzingatia kuwa nacho ni akaunti ya Google. Unapokuwa na akaunti ya Google inakuwezesha kupata huduma mbalimbali ikiwemo kuwa na barua pepe.

SOMA PIA  Tecno kuzindua Spark 5 Pro yenye memori kubwa

Kama tayari una akaunti ya Google hatua ya kwanza ya kutengeneza Youtube Channel ni kwa kuingia Youtube na kubonyeza kwenye akaunti yako ya Google ukiwa Youtube utaona wameandika Create a Channel.  

kutengeneza Youtube Channel

Itachukua dakika moja mpaka tatu Youtube Channel yako kufunguka baada ya kuitengeneza ambapo ikishafunguka utaweza kuipendezesha kwa kuweka picha ya Channel yako pamoja na taarifa zingine za muhimu kuhusu maudhui ya channel yako.

SOMA PIA  Skype Kutafsiri Lugha Moja kwa Moja Kwenye Mazungumzo

kutengeneza Youtube Channel

Baada ya hapo utatakiwa kuwezesha Youtube Channel yako kutengeneza mubashara ambapo itakulazimu kuhakiki namba zako za simu ili uweze kutumia huduma hii.

kutengeneza Youtube Channel

Youtube huanza kumlipa mtu pale ambapo atafikisha masaa 4000 ya video zake kuangaliwa pamoja na wafuasi waliojisajili katika Channel yake 1000. Utakapokuwa na vigezo hivi utaingia katika mfumo maalum wa Youtube na kuanza kulipwa kutokana na matangazo yatakayokuwa yanaonyeshwa katika video zako pamoja na idadi ya watu walioziangalia video zako.

SOMA PIA  Jinsi ya kuweka Bold, tide na Italic kwenye Whatsapp

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia pamoja na matumizi yake. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania