fbpx
Intaneti, Maujanja

Kuwa Makini Usifukuzwe Kazi Kisa Mitandao Ya Kijamii!

kuwa-makini-usifukuzwe-kazi-kisa-mitandao-ya-kijamii
Sambaza

Kama huna kitu kizuri  cha kuongea (ku post) katika mitandao ya kijamii usiongee kabisa. Mfano huwezi ukaanza kuongelea vibaya wafanyakazi wenzako facebook –Psss! hata mimi ningefikiria kukufukuza kazi– Hali hii imejonyesha sana kwa watumiaji wa twitter, wanakuoa wanapost vitu vingi kwa siku kuhusiana na ofisi walizopo hivyo inawabaidi kuwa makini

Saa zingine ule uhuru wa kuongea (freedom of speech) unaweza ukakugharimu kwa hiyo ni vizuri kuangaia ni mambo gani tunayaweka wazi katika mitandao ya kijamii.

Asante kwa mitandao ya kijamii sasa tuna sauti ya mabadiliko na ya kujenga katika jamii lakini hiyo sio tija kila mtu inabidi ajue ni sehemu gani (wakati gani) anahitajika kunyamaza –sio kila kitu lazima useme katatika mitandao ya kijamii—

INAYOHUSIANA  Je tunahitaji Anti-virus katika simu za Android? #Maujanja

Unaweza ukashangaa unayosema leo katika mtandao wa kijamiii yakaja kutumika dhidi yako katika mahojiano (interview) yako ya baadae.

kufukuzwa kazi

Vitu Vya Kuviepuka

1. Kulalamika Kuhusu Kazi Yako Kwenye Mtandao Wa Kijamii

Waswahili wanasema chagua kazi baada ya kupata kazi lakini haimaanishi ndio uikandie kazi yako ya sasa katika mitanao ya kijamii. Bosi wake au hata mfanyakazi mwenzako akiona haitaleta picha nzuri. Licha ya hivyoo hata marafiki zako katika mtandao wa kijamii wanaweza wakakushangaa –Unachukia kazi yako?, sisi inatuhusu vipi?– hayo pamoja na maswali mengine yanaweza yakatawala vichwa vyao

2. Kuweka Wazi Taarifa Za Siri Za Kazini katika Mtandao Wa Kijamii

Hilli pia ni la muhimu, lakini je kwani kuna watu wanashindwa hifadhi siri hizi mpaka kuzipeleka katika mtandao wa kijamii? Mfano nikiona umezianika pale alafu mimi ndiye bosi wako, KAZI HUNA.

INAYOHUSIANA  Facebook yaleta Messenger kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 13

3. Kuingia Katika Mitandao Ya Kijamii Muda Wa Kazi

Ndio saa zingine mitandao ya kijamii ina raha yake la msingi ni kila mtu anahitaji kujua ni mda gani afanye kazi a ni upi afanye kazi.  Kushindwa kutofautisha hii inaweza kukuletea matatizo kazini.

4. Usitume Kitu Cha Kijinga Kwa Kutumia Jina La Kampuni

Hii inamaanisha hata ukurasa wako katika huo mtandao wa kijamii inabidi uwe wa kisomi. Angalia kila unachoandika kisiwe na ubaya wowote. Kwa mfano usijaribu kuuza vitu vyako binafsi kwa kutumia jina la kampuni.

5. Usipige Picha Ukiwa Unapata Kilevi Katika Mazingira Ya Kazi

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kujizuia Na Uraibu (Addiction) Wa Kutumia Simu Janja Kila Mara!

Kama wewe ni mpenda pombe (au kilevi kingine) Usipende kupiga picha ukiwa unajilevya katika mazingira ya kazi. Ukipiga picha na kuweka katika mtandao wa kijamii watu wanaweza kukufikiria vibaya.

Yapo mambo mengi mabaya yanayoweza kukufanya ufukuzwe kazi kama vile kufanya ubaguzi, kuongelea mambo ya ngono na kutoa comments za kukera watu (kukosa busara) katika mitandao ya kijamii.  Kumbuka kuna mabosi wengine kabla ya kuwa ajili watu wanawachunguza kwanza.

Hii inamaanisha wanaingia hadi katika mitandao ya kijamii ili mradi kukuangalia tuu maisha yako katika mitandao ya kijamii. Tuambie njia zingine unazozijua ambazo unahisi zinaweza msababisha mtu kufukuzwa kazi. Pia Usisahau kutembelea mtandao wako wa TeknoKonaDotCom kila siku.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*