fbpx
apps, instagram, Mtandao wa Kijamii

Instagram ya Ronaldo: Atengeneza Tsh Bilioni 2 kwa kila post ya udhamini

instagram-ya-ronaldo-atengeneza-tsh-bilioni-2-kwa-kila-post-ya-udhamini
Sambaza

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ametakiwa kukodisha akaunti yake ya mtandao wa Instagram kwa dau nono kwa muda wa mwaka mmoja.

Shirika kubwa la uwekezaji la Marekani lilimpigia simu nyota huyo na kumuahidia kumlipa donge nono la Euro milioni 100 awakodishe kwa kipindi cha mwaka mmoja ukurasa wake binafsi wa mtandao wa Instagram.

Instagram ya Ronaldo

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Ronaldo aliwajibu kwamba atalifanyia tathmini pendekezo hilo.

 

View this post on Instagram

 

Cold days ask for good quality footwear! Check our CR7 Fall/Winter collection. #PLAYFECTIONISM #CR7fw19 #CR7

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on

Ronaldo ana wafuasi wapatao milioni 187 katika mtandao wa Instagram, aliingiza kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 38.2 kutoka shirika hilo.

INAYOHUSIANA  App 5 Muhimu Za Kuwa Nazo Katika Simu Janja yako! #Machi2016

Cristiano Ronaldo ndiye nyota anayeingiza pesa nyingi kupitia akaunti yake ya Instagram, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika post za Instagram 49 kwa wastani alilipwa  kiasi cha Dola 975,000 kwa kila posti moja ambapo kwa mwaka mzima idadi inafikia Dola 47.8 Milioni (Takribani TShs Bilioni 109.8).

Soma zaidi habari na maujanja ya apps mbalimbali -> Teknokona/Apps

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.