fbpx
Android, apps, Play Store

Usalama: Hizi ni apps za kuziondoa kwenye simu yako. #Adware #Android #iOS

usalama-apps-za-kuziondoa-kwenye-simu-yako-adware-matangazo
Sambaza

Watumiaji wa Android wamepewa orodha ya apps za kuziondoa kwenye simu zao kwa sababu za kiusalama wa data na kuondoa matangazo yanayotokea sehemu zisizohusika kwenye simu zao.

Ushauri huo umetolewa na watafiti kutoka ESET ambao wamegundua app 42 kwenye soko la Google Play Store ambazo zimekuwa zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi – adware. Mfumo huo una sababisha betri ya simu kuisha haraka, utumiaji wa data – intaneti na ata kuchukua taarifa zako binafsi kwenye simu.

INAYOHUSIANA  VLC 3.0: VLC waleta sasisho kubwa zaidi, Download toleo jipya kwa simu, kompyuta n.k
apps za kuziondoa google playstore android 1
Apps za kuziondoa: Apps hizi zinaingilia mfumo wa kawaida wa kufanya kazi wa simu kwa kuweza kuonesha matangazo sehemu mbalimbali zisizohusika kwenye simu yako

Baada ya utafiti wa ESET kuweka wazi Google waliondoa apps hizo kwenye soko lao la Apps, ila inakuitaji wewe kuziondoa mwenyewe. Pia kuzifahamu ni muhimu kwa watu ambao wanatumia masoko mengine ya apps nje ya soko la Google Play Store. Apps hizo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 8.

Apps hizo ni: Smart Gallery, SaveInsta, Mini lite for Facebook, Free Radio FM Online, Free Video Downloader, Free social video downloader, File Downloader, Water Drink Reminder, Smart Notes for You, DU Recorder, Tank classic, Heroes Jump, Solucionario, Ringtone Maker, Video downloader, Ringtone Maker Pro, Basketball Perfect Shot, HikeTop+, MP4 video downloader, Flat Music Player, Free Top Video Downloader.

INAYOHUSIANA  Instagram yaleta Chaneli kwa ajili ya Video za matamasha

Apps hizo zinauwezo wa kuonesha matangazo ata kama simu imefungwa (locked) kitu ambacho huwa kinapigwa na Google, kwani kufanya hivyo kuna sababisha utumiaji mkubwa wa betri na nje ya makubaliano yao na watengenezaji wa apps.

Baadhi ya apps hizo zipo pia kwenye soko la apps la iOS kwa ajili ya simu za iPhone ila inaonekana kwa iPhone bado apps hizo hazifanikiwa kuwa athari kubwa ukilinganisha na kwenye simu za Android.

INAYOHUSIANA  Watumiaji wa App Store Watumia zaidi ya Tsh Trilioni 2 (Bilioni $1.1) Kipindi cha Sikukuu

Pitia orodha vizuri na kama kuna app bado unaitumia unashauriwa kuiondoa.

Chanzo: Express.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |