fbpx
Android, apps, simu, Uber

Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi

uber-waanza-na-india-kutoa-toleo-dogo-kabisa-la-programu-tumishi
Sambaza

Uber ni kampuni inayofahamika sana ulimwengu kutokana na shughuli zake za kuita usafiri uje ukuchukue kwa njia ya kidijitali kupitia programu tumishi na usafiri ukafika baada ya muda fulani.

Uber imetoa toleo jipya la programu tumishi ambayo kimsingi ni ndogo kwa ukubwa na kuweza kufanya kazi sehemu ambayo inapatikana 2G; hapa nazungumzia Uber Lite.

Kwanini Uber wamzindua Uber Lite nchini India kwanza?

Nchini India ni sehemu ambayo Uber bado ina wateja wengi vilevile ndio soko kubwa na pekee ambalo Uber limebakiwa nalo katika bara la Asia. Mpaka sasa India ina watu zaidi ya 1.3 bilioni.

INAYOHUSIANA  App 5 Za Kuingia Nazo Mwaka 2016

Yalyomo kwenye Uber Lite.

a) Sifa kuu ya Uber Lite ni kutokuwa kubwa; ina ukubwa wwa chini ya MB 5 ukilinganisha na programu tumishi mama ya Uber yenye ukubwa wa MB 181.4. Kwa maana hiyo Uber Lite ni nyepesi katika ufanyaji wake wa kazi na inachukua nafasi ndogo kwenye simu.

b) Kufanya kazi mpka kwenye 2G. Programu tumishi nyingi zinakubali kufanya kazi iwapo mnara unasoma 3G. Hapa tafsiri yake ni kwamba hata yale maeneo ambayo 3G kupatikana ni tabu bado utaweza kutumia Uber Lite kwa 2G.

INAYOHUSIANA  FUNUNU: iPhone SE Ijayo Itakua Na Umbo La iPhone 8!
toleo dogo kabisa
Uber Lite inayofanya kazi hata kwenye 2G yazinduliwa kwenye moja ya taifa lenye watu wengi duniani.

c) Uber Lite inatumia GPS ya dereva kuweza kujua inayofuata anapoweza kuhitajika hivyo hakuna haja ya dereva kuandika andika sehemu anapokwenda.

Kilichoondelwa ni ramani pamoja na gari zinazoonekana mara tu unapofungua ile programu tumishi kuu ya Uber; menyu mpya ya kwenye Uber Lite haina vitu vingi ingawa kipengele cha ramani unaweza ukachagua kuona au ukaacha zisionekane.

Uber Lite inapatikana kwa wanaotumia Android na kwa sasa inapatikana nchini India tu lakini ikitegemewa kuanza kupatikana katika nchi nyingine duniani katika siku za usoni.

Vyanzo: Gadgets 360, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    June 13, 2018 at 9:27 pm

    […] post Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi appeared first on TeknoKona Teknolojia […]