Dunia kote huduma zinarahisishwa zaidi kupitia teknolojia kwa sasa, na kampuni ya Azam Group haipo nyuma. Imekuja na app itakayotumika katika simu janja ili kumrahisishia mteja wake kuweza kununua na kufikishiwa bidhaa dukani kwake kwa njia rahisi na ya haraka zaidi.
Programu hiyo iliyopewa jina la Sarafu kwa sasa inapatikana kwa simu za mfumo wa Android, imeweka uwazi mzuri kwa wateja wote wenye kutaka kununua au kujua bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya Azam Group.
Aidha inamrahisishia mteja wa reja reja kununua bidhaa mbalimbali za Azam kwa bei ya chini kuliko kununua kwa muuzaji wa Jumla.
Uzuri mwingine wa kutumia App ya Sarafu ni kuona bidhaa zote zilizokuwepo na bei yake bila ya kuwa na wasiwasi wa kuwepo bidhaa fulani au la. Mteja anapoamua kununua bidhaa anazohitaji ndani ya saa ya kadhaa atapokea mzigo wake.
Kwa mteja atakayeagiza mzigo kuanzia saa moja ya asubuhi mpaka saa 6 ya mchana ataupata mzigo wake kwa siku hiyo hiyo na yule atakayeagiza baada ya saa sita ataupata siku inayofuata.
Huduma hii ya kununua na kupelekewa mzigo wako pale ulipo ni kwa bidhaa zinazoanzia TShs 70,000/. Huduma hii kwa sasa ni kwa wateja wa Dar es Salaam na hakuna malipo ya usafiri pale unapoletewa mzigo wako.
Fursa zipo nyingi ukijiunga na Sarafu App ikiwemo ya mteja anayefanya manunuzi ya mara kwa mara kuweza kupata nafasi ya kupata mkopo mpaka wa milioni moja ambao ataweza kununulia bidhaa zilimo ndani ya Sarafu.
Ambapo mkopo huo ataweza kuulipa katika muda atakaopangiwa. Pia inatoa fursa ya kupata Updates/taarifa mpya tofauti kuhusu bidhaa mpya zinazoingizwa sokoni.
Namna ya kuwa na App ya Sarafu na kujiunga kupata huduma hizo fungua link hapo chini.
BONYEZA HAPA
Soma kuhusu apps mbalimbali nyingine -> Teknokona/Apps