fbpx

Oppo yashehrekea pamoja na uzinduzi wa bidhaa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tukitaka kujua makampuni ambayo yanafanya vizuri kwenye tano bora basi Oppo haiwezi kukosekana kwenye orodha na hivi karibuni wamesheherekea mafanikio waliyoyapata yaliyoambatana na uzinduzi wa bidhaa.

Bidhaa za Oppo si haba zimefika Afrika na kwa hakika hata sehemu nyingine duniani vitu vyao vinauzika. Kampuni hiyo huko Shanghai iliandaa tamasha mahususi kabisa kwa ajili ya kile walichoweza kufanikiwa.

Sababu ilivyowafanya Oppo kufurahia mafanikio kiasi cha kuandaatamasha ni kuweza kuuza bidhaa takribani 100 milioni zote zikiwa na teknolojia ya kuchaji kwa haraka sana.

uzinduzi wa bidhaa

Bidhaa zote 100 milioni ambazo zimeshauzwa zina teknolojia ya kuchaji betri kutoka (0-75)% ndani ya dakika 30.

Ktika tamasha hilo pia Oppo walilitumia kutambulisha kifuko cha kukinga Oppo R17 Pro kutodhurika ikianguka, vipeperushi vidogo vidogo kuhusu NFC na kimemeshi cha ziada ambacho kina 10000mAh inayotoa 5V/10A.

uzinduzi wa bidhaa

Bidhaa zilizozinduliwa kwenye sherehe ya Oppo kufanikiwa kuuza vifaa vya kidijiti takribani milioni 100 kwa idadi.

Ni wazi kuwa wana kila sababu ya kujivunia kwa kile ambacho wamekifanikisha. Kimemeshi hicho cha ziada kitauzwa kwa karibu $60|Tsh. 138,000.

Vyanzo: GSMArena, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kuhusu Google Pixel 3a na 3a XL sio fununu tena
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.