fbpx

IPP kuanzisha kiwanda cha simu za mkononi nchini

0

Sambaza

Kampuni ya IPP kupitia Mwenyekiti Mtendaji wake imetangaza kujenga kiwanda cha simu bora na za bei nafuu nchini.

Sambamba na simu, kiwanda hicho pia kinatarajia kutengeneza vifaa mbalimbali vya kielektroniki kama vipakatalishi (kompyuta, tabiti), spika zisizokuwa na waya, spika za masikioni pamoja vifaa vya nyumbani.

Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam na uwekezaji wake unakadiriwa kuwa Tsh. bilioni 11.5. Pia, kitakuwa na uwezo wa kuzalisha simu za mkononi 1,200 kwa siku, kuajiri watu zaidi ya 2,000 ( watu wenye ulemavu watapewa kipaumbele kwenye ajira).

kiwanda cha simu

Kampuni hiyo itaitwa IPP Touchmate Ltd na imejiandaa kukabiliana na ushindani wa kampuni nyingine zinazoingiza bidhaa kama hizo Afrika.

IPP Touchmate Ltd itatengeneza simu ambazo zina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja, pamoja kutumika kuchajia simu nyingine zikiwa ni maalum kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hususani vijijini.

Kwa uchache

Imeelezwa kioo cha simu janja kitakuwa na urefu wa inchi 5.72, zitakuwa na mfumo wa 4G, kutoingia maji wala kuvunjika, kudumu na chaji kwa muda wa siku moja mpaka mbili (iwapo imetumika kwa matumizi ya kawaida).

Zitakuwepo tabiti zinazotumia nishati ya Jua kila moja ikiwa imeweka vitabu vya kidijitali (e-books) kulingana na mitaala ya masomo katika shule za mingi na sekondari mahususi kwa ajili ya shule za vijini ambapo umeme ni wa shida.

Kompyuta zitakazotengenezwa zitauzwa kwa mkopo Tsh. 500,000 kila moja lakini mwanafunzi wa chuo atalipa kwa awamu pesa huyo.

Uzalishaji wa bidhaa hizo unatazamiwa kuanza katika siku 90 zijazo huku asilimia kuwa ya wafanyakazi watakuwa ni Watanzania (wakiwemo walemavu) na wakufunzi kutoka Touchmate Dubai watakaofundisha wafanyakazi kwa muda wa miezi sita.

Ujenzi wa kiwanda hicho ni ushirikiano na kampuni ya Touchmate iliyoko Dubai yenye uzoefu wa miaka 30 wa kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama simu janja, tabiti, kompyuta na vifaa vya nyumbani.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Halotel watangaza vifurushi vipya
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.