Je kuna simu hautaitumia kwa muda mrefu? au ni betri la ziada ambalo unataka kulihifadhi kwa muda mrefu kwa usalama… leo jifunze jinsi ya kuhifadhi betri la simu kwa muda mrefu bila kuathiri ubora wake.
Muhimu;
- Kama una simu na unampango wa kutoitumia kwa muda mrefu basi hii ni njia bora zaidi ya kuhakikisha betri lake linakaa katika ubora mzuri kwa muda mrefu.
- Si salama kuacha betri kwenye simu isiyotumika kwa muda mrefu
Hatua zifuatazo zikitumika basi utaweza kuhifadhi salama betri la simu yako ata miezi na miezi bila ya betri hilo kuharibika.
Hatua ya kwanza
Hakikisha kiwango cha betri hilo kipo angalau asilimia 40%, kiwango cha chaji kisipungue au kuzidi sana zaidi ya hapo. Chomoa betri hilo kutoka kwenye simu hisika.
Hatua ya pili
Hifadhi betri katika mfuko wa plastiki usiopitisha hewa. Funga na hakikisha hewa haiingii, na jitahidi unavyoweza kuhakikisha hewa nyingi haibaki ndani ya mfumo huo.
Hatua ya tatu
Hifadhi kwenye jokofu (friji) yenye kiwango cha ubaridi wa angalau digrii 15 za sentigredi. Hakikisha hakuna hewa inayoingia kwenye mfumo ulioweka betri na ni vizuri usiweke karibu na kitu cha kula ingawa kama umefunga vizuri mfuko wake basi hakuna tatizo.
Betri lako litakuwa salama kwa miezi na miezi bila kupoteza ubora wake.
Hatua ya nne
Pale utakapotaka kulitumia. – Litoe kwenye mfuko na tumia kitambaa kikavu kufuta unyevu nyevu wa baridi. Kisha liache likae sehemu yenye hewa kwa muda ili liweze kupoa. – inaweza ikawa dakika 30 – lisaa limoja, hakikisha ubaridi umeisha na betri ni kavu kabla ya kulitumia.
Weka betri kwenye simu na kisha washa. Tayari utaweza kutumia betri lako kama kawaida.
Soma maujanja mengine mbalimbali -> TeknoKona/Maujanja