fbpx

Vinara wa matumizi ya sarafu zisizoshikika

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Leo hii kuna mataifa ambayo yanatumia kisawasawa teknolojia inayoruhusu matumizi ya sarafu zisizoshikika na katika hali ya kawaida nchi nyingi bado hazijakubali mfumo huo lakini watu wanajiingizia kipato.

Serikali/mamlaka husika katika nchi mbalimbali zimekuwa nzito kuubali au kutambua uwepo wa teknolojia ambayo imetawaliwa na matumizi ya intaneti kuwekeza pesa halafu baada ya muda fulani thamani ya uwekezaji inaongezeka na kutengeneza faida, kwa lugha ya Kiingereza inaitwa “Blockchain“.

Kwanini blockchain haipewi uzito wa aina yake?

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na hata baada ya kuhudhuria makongamano mbalimbali kuzungumzia blockchain sababu kubwa ni:-

Uaminifu. Hii inatokana na kwamba haijulikani miamala inafanyika kivipi na baadae kuweza kubadilishwa kuwa pesa kamili hitimisho lake kuwa pesa kuweza kuhamishwa akaunti ya mtandaoni na kuingia kwenye akaunti halisi ya mteja kupitia benki.

Jambo hilo linasababisha serikali kuweza kuingia na kujua kinachofanyika hatimae kutengeneza mifumo rasmi kitu ambacho kitawezesha mamlaka husika kupata kodi.

matumizi ya sarafu

Aliyetengeneza mfumo wa mzima wa “Blockchain” jina lake linafahamika lakini sura yake haifahamiki mpaka leo.

Nchi zinazoongoza kujipatia kipato kutokana na matumizi ya sarafu zisizoshikika.

Shukrani kwa Satoshi Nakamoto ambae alibuni na kuleta kwa ulimwengu kitu hicho ambacho kimezaa sarafu nyingi tu za kidijitali zikiwemo Bitcoin, Munero na nyinginezo.

Nchi zinazotumia sarafu za kidijitali kujipatia kipato na Bitcoin ndio inaongoza kwa kutumiwa katika nchi nyingi.

Ingawa Tanzania matumizi ya teknolojia hiyo bado yapo chini sana (hayajashamiri) lakini tumeshika nafasi ya 43 huku jumla ya miamala ya thamani ya $2M ikiwa imefanyika.

Kama ulikuwa hujafahamu Tanzania ina jumuiya (Blockchain Tanzania) ambayo inalenga kufahamisha watu kuwa kitu hicho kipo na kinaweza kuwa moja ya vyanzo vya mapato.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uber yaingia kwenye ulingo wa kumilikiwa na wengi
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|