Kutokana na janga la hatari la virusi vya Corona linalotikisa dunia tumeona kampuni nyingi zimeweza kufunga ofisi zao na kufanya kazi kupitia mtandao wakiwa nyumbani. Jambo hili limeweza pia kutoa fursa kwa baadhi ya kampuni zinatoa huduma za mazungumzo kwa njia ya picha mnato kupitia mtandao.
Kampuni nyingi zimeweza kupata fursa ya kuuza progamu zao zinatoa huduma hizo lakini chache kama Zoom zimeweza kupata watumiaji wengi duniani kote tangu ugonjwa huu ulipoanza.
Google wana programu yao inayoitwa Google Meet iliyoanzishwa mnamo mwaka 2017 ambapo ilikuwa ni ya kulipia sasa inapatikana bila malipo kabisa. Programu hii ni ya kufanya mikutano ambayo wanafunzi, wafanyakazi au mtu yeyote anaweza kutumia kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wenzake kuhusu elimu, kazi, n.k.
Programu Hii sasa imeweza kuunganishwa Moja kwa moja kwenye akaunti za watumiaji wa GMAIL kama inavoonekana hapo chini Nimepata masasisho mnamo 16/05/2020. ambapo mtu anaweza akaanzisha ama kujiunga kwenye mazungumzo kwa njia ya picha jongefu.
Jinsi ya kuandaa mkutano
- Bonyeza kwenye Start Meeting iliyopo upande wa kushoto Ukiwa ndani ndani ya barua pepe yako
- Baada ya hapo utaletewa ukurasa kama huu hapo chini ambapo moja kwa moja utakuwa umeshaanzisha mkutano ambao unaweza ukajiunga (join) ama ukaonyesha kitu/taarifa (present) muonekano wa kifaa unachotumia kama ukihitaji.
- Baada ya kubonyeza “Join Now” unakuwa umeingia moja kwa kwa moja kwenye mazungumzo yako na utapewa ujumbe wa kuwaalika rafiki zako, na kukusanya taarifa za kuwawezesha watu wako kuzitumia wakitaka kujiunga.
- Kama utatataka kuwaalika rafiki zako moja kwa moja kwa njia ya email basi utabonyeza “Add People” halafu utaandika barua pepe za watu unaotaka kuwaalika katika mazungumzo kisha utabonyeza “Send Email“.
- Watu wako watapokea ujumbe wa mualiko wa meeting katika barua pepe zao kama inavoonekana hapo chini na endapo akibonyeza kwenye “Join Now” ataweza moja kwa moja kuingia kwenye mkutano tayari kwa ajili ya majadiliano.
Pia huduma hii inapatikana moja kwa moja kwa kutembelea ukurusa wa Google Meet na kuweza kuanziasha na kujiunga mazungumzo mubashara.
