fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao wa Kijamii Teknolojia

SnapChat Kuzuia Manunuzi Ya ‘Lense’!

SnapChat Kuzuia Manunuzi Ya ‘Lense’!

Spread the love

Bado kidogo mtumiaji wa snapchat ambae anapenda ku’post’ picha na video zenye manjonjo manjonjo (effects) atakuwa hana uwezo wa kununua lense hizo tena. Snapchat mbioni kuzuia manunuzi hayo na hii itajumuisha lense zile za kwenye mtandao wa snapchat na zile za kwenye mitandao mingine ya makampuni ya nje (ya snapchat).

Soko la snapchat la lense lilikuwa likimuwezesha mtumiaji wa snapchat kuweza kununua lensi hizi kwa dola 0.99 za kimarekani kwa kila lensi moja. Mabadiliko haya yatakua katika hatua ya kutekelezwa mwishoni mwa juma hili.

SOMA PIA  Vitu Kwenye Windows Ambavyo Microsoft Hawawezi Kuvijibu!

Licha ya kufanya mabadiliko haya, haimaanishi kuwa snapchat itakuwa haina matumizi ya lense. Lense zitakuwepo kama kawaida ila zitakuwa ni chache tuu. Na kwa mtu ambae alinunua lensi zake toka mwanzo basi ataweza kuzitumia hata mabadiliko haya yatakavyofanywa. Kwa wale ambao hawakufanya manunuzi ya aina yeyote snapchat itawawezesha kupata lensi kadha wa kadha zisizozidi 10 kwa siku (bure)

Lense Maarufu Katika App Ya SnapChat Ikiwemo Na Ile Ya 'Upinde Wa Mvua'

Lense Maarufu Katika App Ya SnapChat Ikiwemo Na Ile Ya ‘Upinde Wa Mvua’

Kampuni (snapchat) limesisitiza kuwa watu wategemee kuona lense nyingi ambazo zilikuwa bure katika soko la lensi na pia wasitegemee sana kwamba watapata zile lensi ambazo zilikuwa ni maarufu sana na zinapendwa. Kampuni kama kampuni litakuwa na tabia ya kubadilisha badiilisha mpangilio wa lense hizo mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna bora zaidi.

SOMA PIA  Tanzania Kushirikiana na Toshiba katika Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi

Mpaka sasa ili kuwa na uhakika wa kuwa na lense mbalimbali unazozitaka au kuzipenda itakubidi uzishushe kutoka katika soka hilo la lensi kwa haraka kabla ya Snapchat haijafanya mabadiliko haya. Kumbuka zile ulizonunua hazitaguswa!

SnapChat ilitambusha lensi zake za kusogea sogea (animated)  mwaka jana na jambo hilo lilipata umaarufu wa haraka baina ya watumiaji wa Mtandao huo wa kijamii. Watumiaji katika mtandao huo ni wengi na wamekuwa wakiongezeka kwa kasi sana

SOMA PIA  Mapato ya Huawei yaporomoka zaidi, vikwazo vya Marekani vinang’ata biashara

Kwa Habari Mbalimbali Za Mtandao Wa Kijamii Wa SnapChat Bofya Hapa

Tuambie wewe kama mwana teknolojia unayachukuliaje mabadiliko haya ya mtandao wa kijamii wa snapchat, tuambie sehemu ya comment hapo chini. Usisite kutemhbelea mtandao wako pendwa wa TeknokonaDotCOm kila siku ili kupata habari moto moto za kiteknolojia.TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania