fbpx
Android, apps, Facebook, Teknolojia, whatsapp

Messenger Rooms kwenye WhatsApp

messenger-rooms-kwenye-whatsapp

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Nianze na swali, ni kwa kiasi gani kipindi hiki unawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki? Si ajabu ukafurahishwa na hili kwa kitendo cha Facebook kuweka Messenger rooms ndani ya WhatsApp.

Kwa kipindi hiki ambacho si jambo zuri sana kukutana na watu ana kwa ana bila ya kuwa na tahadahri ya kiafya basi ni vyema tukafikiria njia mbadala za kuweza kuonana na watu kwa njia ya kidijiti.

Mwezi jana Facebook walitambullisha “Messenger Rooms” na kukiruhusu kufanya kazi siku chache tuu zilizopita ndani ya Facebook messenger  lakini sasa kipengele hicho kimesogezwa kwenye WhatsApp beta toleo 2.20.163 kwenye Android pekee.

Je, Messenger rooms ni nini?

Hiki ni kipengele ambacho kinamuwezesha mtu anayetumia Faccebook Messenger kuweza kuwasiliana na jamaa zake kwa njia ya picha mnato (jongefu). Hapo mtumiaji ataweza kuwasiliana na marafiki zake hadi watu hamsini (50) kwa wakati mmoja.

Messenger rooms
Ongea na jamaa zako wa kwenye Facebook messenger kupitia mlango wa WhatsApp.

Je, inapatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp?

Ukiacha kwamba kwa sasa inapatikana kwa wanaotumia simu janja za Android tu lakini kipenge hicho pia kimeruhusiwa kwenye baadhi ya watu na nchi pia lakini tutarajie kukiona katika siku za usoni kikipatikana kwa watu wengi zaidi wakiwemo wale wanaotumia rununu zenye iOS.

INAYOHUSIANA  Mimicker Alarm: Microsoft Waja na App Matata ya Kukuamsha Asubuhi, ni App itakayokusumbua hadi uamke!

Inawezekana inakuaje Facebook ina uhuru wa kupeleka maboresho kwenye WhatsApp? Hii ni kwa sababu Februari 19 2014 alinunua WhatsApp na hivyo kuwa chini yake.

Vyanzo: GGSMArena, WABetaInfo

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|