fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Gmail Go

Gmail Go kwa ajili ya simu yenye memori ndogo

Spread the love

Ukiwa unatumia simu janja basi barua pepe ni ufunguo wa kuwa na uwezo wa kupakua programu tumishi mbalimbali kutoka sokoni. Kwenye Android ni lazima uwe na akaunti ya Gmail na kwa lugha rahisi tuu programu tumishi husika itakuwezesha kuandika/kusoma jumbe ulizotumiwa kirahisi kabisa.

Mpaka leo kuwa simu janja ambazo zina memori na RAM ndogo jambo ambalo linafanya simu kuzidiwa uwezo na ufanisi wake wa ufanyaji kazi kuwa mdogo kiasi kwamba mtu anapata kadhia kutumia rununu. Jambo hili ndio linasababisha makampuni mengi kutengeneza programu tumishi ambazo si kubwa hivyo kufanya simu kutekeleza majukumu yake vizuri tuu.

SOMA PIA  Xbox kuja na app mbali mbali kama Netflix, Apple Tv, YouTube

Google wameendelea kuja na programu tumishi mbadala mahususi kwa zile rununu zenye memori (diski uhifadhi na RAM) ambapo hivi sasa Gmail Go inapatikana kwenye Playstore. Kimsingi Gmail Go imetengenezwa ili kutoathiri ufanyaji kazi wa simu zenye uwezo mdogo. Mbali na hilo toleo la “Gohakuna kitufe cha Google Meet na muonekano wake ni wa kawaida ila unafanana na programu tumishi kuu.

memori ndogo

Muonekano wa Gmsil Go-programu tumishi ya kusoma ujumbezilizotumwa kwenye barua pepe mahususi kwa simu zenye memori ndogo.

Kama unatumia simu janja ambayo ni Android na ina memori ndogo au hata kama rununu ina uwezo wa juu lakini hutaki memori ijae haraka basi ni vyema ukapakua Google Go, Facebook Lite, Messenger Lite, Twitter Lite na sasa Gmail Go kwa ajili ya matumizi ambayo hayataathiri ufanisi wa kifaa husika.

Vyanzo: GSMArena, Firstpost

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania