fbpx

Samsung, simu, Teknolojia

Hii ndio Samsung Galaxy A42 5G

hii-ndio-samsung-galaxy-a42-5g

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Samsung wameendelea kutoa simu janja ambapo mwezi Machi 2020 ilitoka Galaxy A41 lakini Septemba mwaka huu wakaona inafaa kuzindua toleo linalofuata ambalo kimsingi lina memori kubwa, kamera zenye ubora zaidi pamoja na mambo mengineyo.

Samsung Galaxy A42 5G ilizinduliwa bila ya sifa zake kuwekwa wazi lakini kwa mujibu wa chapisho kutoka kwa walioitengeneza undani wa rununu husika umeweza kufahamika. Sifa za simu janja husika zinaeleza mengi kuhusu bidhaa yenyewe:

Muonekano+Kipuri mama

Kwa mbele una kioo chenye umbo la herufi “U”, kidoti mithili ya tone la maji kwenye eneo la kamera ya mbele, urefu wake ni inchi 6.6 HD+Super AMOLED. Kipuri ni  8 kwa 1-Qualcomm Snapdragon 750G ambapo kasi yake ni 2.2GHz.

INAYOHUSIANA  Mauzo ya bidhaa za Apple zenye rangi nyekundu

Kamera+Betri

Upande wa nyuma ina kamera 4+taa ya kuongeza ung’avu wa picha; MP 48, MP 8 na mbili zina MP 5 kila moja. Kamera ya mbele ambayo kazi yake ni zile picha za kujipiga mwenyewe ina MP 20. Kuhusu betri ina jumla ya 5000mAh, nguvu ya 15W kwa ajili ya teknolojia inayosaidia kujaza chaji kwa haraka.

Galaxy A42
Mpangilio wa kamera kwenye Samsung Galaxy A42 5G.

Memori

SImu janja yenye kipuri mama cha uwezo wa juu unaenda sambamba na RAM hivyo kwenye Samsung Galaxy A42 5G ina toleo 3 za memori; GB 4, GB 6 na GB 8. Upande wa diski uhifadhi ni GB 128 lakini ikiwa na uwezo wa kukubali memori ya ziada mpaka TB 1.

INAYOHUSIANA  Serikali ya Uchina na magari yanayotumia umeme

Mengineyo

Inatumia teknolojia ya 5G, rangi zake ni Nyeusi, Nyeupe na Kawawia. Teknolojia ya kutumia alama ya kidole ipo ndani ya kioo, uzito wake ni gramu 190, Bluetooth 5.0, USB Type-C. Kwa toleo lolote ambalo mtu atanunua diski uhifadhi itakuwa ya GB 128 hivyo tofauti itakuwepo kwenye RAM na rangi tu.Galaxy A42

Tayari imeshazinduliwa lakini bado haijaingia sokoni mpaka mwezi Novemba huko Ujerumani na gharama yake inakkadiriwa kuwa zaidi ya $430|Tsh. 989,000. Kiujumla hii ni simu janja ya uwezo wa hali ya juu kulingana na sifa zake. Vipi wewe maoni yako?

Vyanzo: Gadgets 260, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*