Pengine utakua umeshawahi kuisikia kampuni ya teknolojia ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao (fintech) inayojulikana kama NALA.
Kampuni hii inamilikiwa na mtanzania na inajikita sana katika kurahisisha utumiaji na upokeaji wa hela ndani na nje ya nchi.
Mpaka sasa ina matawi mengi katika nchi tofauti tofauti kama vile uingereza, marekani, Uganda n.k ambapo utaweza kutuma na kupokea hela kwa gharama nafuu.
Selcom kwa upande mwingine ni kampuni nguli sana hapa Tanzania na imekua ikirahisha jinsi ya kufanya malipo ya aina mbali mbali kama vile luku, maji n.k
Kampuni hizi mbili zimeungana ili kuhakikisha kuwa inarahisisha utumaji wa pesa ndani ya Tanzania.
Sasa basi watumiaji wa App ya NALA waliopo nje wana uwezo wa kuweza kutuma pesa na zikaingia katika mifuko mbali mbali ya benk na hata iel ya simu kwa urahisi kabisa.
Kwa sasa kampuni ya NALA ipo ndani ya nchi 7 na bado inazidi kusogea katika nchi mbalimbali kwa mpaka mwakani wana lengo la kuwa wamefikia Zaidi ya nchi 12.
Uzuri wa kitu kama hiki ni kwamba kuna hati hati kubwa sana huko mbeleni mtu wa ulaya au marekani akawa analipa bili za huku Tanzania moja kwa moja kwa urahisi kabisa.
Moja kati ya kampuni za kiteknolojia ambazo zinakua kwa kasi sana kutokea Tanzania ni NALA, insatahili sifa zote.
CHANZO: The Citizen
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hili umelipokeaje? Je ushawahi kutumia huduma ya NALA?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.