fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

simu Teknolojia Uchambuzi Xiaomi

Unafahamu sifa za Xiaomi Poco X3 NFC?

tecno

Kutokana na sababu mbalimbali unaweza ukawa unabadilisha simu janja mara mbili hadi tatu kwa mwaka mzima na si suala la kufichika kuwa ushindani kwenye biashara ya vitu vya kidijiti ni mkubwa sana.

Mwezi Septemba mwaka huu kuna simu nyingi tuu ambazo zimetoka na mojawapo ni Xiaomi Poco X3 NFC ambapo kampuni husika inaonekana kufanya vizuri kwenye soko la ushindani hata kuwepo kwenye tano bora ya mauzo za bidhaa.

Sasa kuna Xiaomi Poco X3 NFC ambayo ilizinduliwa Septemba 7 ikiwa imejaa sifa za kuvutia inayoendana na nini wateja wanataka. Undani wa rununu husika ni kama ifuatavyo:-

Kipuri mama/Muonekano

Ni simu ya mguso yenye kioo cha Gorilla (hakivunjiki kirahisi) chenye nchi 6.67 (1080x2400px) lakini uzuri wa simu janja yoyote unategemea na kiungo ambacho kinafanya ufanisi wa simu uwe mzuri; nazungumzia kipuri mama ambapo rununu husika imwewekwa Qualcomm Snapdragon 732G.

Kamera

Siku hizi mtu akununua simu janja anakuwa anajua anataka kamera yenye sifa gani; Poco X3 NFC ina jumla ya kamera nne nyuma ambazo zina MP 64, MP 13 halafu mbili za mwisho zote ni MP 2 kila moja bila kusahau uwepo wa “Taa ya mwangaza“. Kwenye uso wa mbele kuna kamera moja yenye MP 20.

Xiaomi Poco X3

Mpangilio wa kamera kwenye Poco X3 NFC.

Betri

SOMA PIA  App ya kujitegemea ya Instagram Direct kuondolewa!

Moja ya vitu ambavyo inatufanya tuwe na simu zaidi ya moja ni utunzaji wa chaji kwa rununu husika. Xiaomi Poco X3 NFC ina 5160mAh, teknolojia ya kuchaji haraka (33W); kuchaji mpaka 62% inachukua nusu saa, kufika 100% ndani ya dakika 65.

SOMA PIA  Nokia kuingiza dola 3.48 kwa kila simu yenye 5G

Memori/Bei

Moja ya kipengenele ambacho wateja wengi wanavutiwa nacho kutokana na kwamba simu zetu zinaweza kufanya vitu vingi mbali na kufanikisha mawasiliano. Kwenye rununu hii ina GB 64, GB 128, RAM GB 6 lakini pia inawezekana kuweka diski uhifadhi ya ziada yenye ukubwa wa mpaka GB 256. Gharama yake inaanzia $229|zaidi ya Tsh. 526,700 na $379|zaidi ya Tsh. 871,700 bei ya kuagiza.

Xiaomi Poco X3 NFC

Ina 3G, 4G, LTE, Bluetooth 5.1,sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, 2.0 USB-C, OTG, teknolojia ya kutumia alama ya kidole, sehemu ya kuchoka kadi mbili za simu, Wi-Fi.

Hao ndio Xiaomi na simu janja mpya ambayo tayari imeshaingia sokoni. Vipi msomaji wetu umevutiwa nayo? Tupe maoni yako.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360.

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania