fbpx

Muhstakabali wa kuona BURE chaneli za ndani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Bado mambo ni magumu na wengi wetu hatupati matangazo ya chaneli za ndani (kwa Tanzania) na hivyo kukosa taarifa mbalimbali kutoka kwao, yote hii mzizi wake ni kuweza kuona BURE chaneli za nyumbani.

Visimbuzi takribani vitatu mpaka hivi leo havirushi matangazo ya chaneli za ndani baada ya TCRA kuwataka kutii masharti ya vibali walivyovilipia ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

Kitu ambacho kinachozuia makampuni wasirushe matangazo ya chaneli za ndani.

Iwapo unatumia king’amuzi cha ZUKU, DSTV au AZAM basi utakuwa ni mmoja kati ya wateja wengi ambao hawapati matangazo ya ITV, Chaneli 10, Star TV, EATV, n.k lakini je, unafahamu mpaka leo kwanini bado hatupati matangazo ya chaneli za ndani? Sababu ni rahisi sana.

Leseni walizolipia DSTV, ZUKU na AZAM TV ni kwa ajili ya kulipia chaneli nyingine (kulingana na vifurushi vyao) ikiwemo TBC 1. Hivyo, ili kuweza kurusha matangazo ya chaneli ya ndani itabidi warudi TCRA na kwenda kulipia leseni tofauti na waliyonayo sasa.

Wanaotumia ving’amuzi vya Startimes vinavyotumia antena za ndani wanaona chaneli za ndani bila kulipia kwa mujibu wa kibali walichonacho.

 kuona bure

Sakata lakuonyesha chaneli za ndani bila malipo.

Hatuna budi kuwa wavumilivu mpaka pale watakapoamua kulipia leseni tofauti au muafaka kati ya TCRA na makampuni hayo yatakapoafikiana.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Halotel watangaza vifurushi vipya
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.