fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPad IPhone

FUNUNU: Apple Katika Mpango Wa Kuondoa Kitufe Chao Kilichozoeleka!

FUNUNU: Apple Katika Mpango Wa Kuondoa Kitufe Chao Kilichozoeleka!

Spread the love

Inavyosemekana kampuni la Apple linafanya juu chini ili kuondoa kitufe chake kilichozoeleka kile cha kukurudisha katika ukurasa wa nyumbani mara nyingi kinajulikana kama ‘Home Button”  katika simu zake zijazo

Apple walivyoleta simu za iPhone rasmi mwaka 2007, walibadilisha soko zima la simu kwa ujumla. Watengenezaji simu nao wakabadilisha aina za ufikiriaji katika kubuni simu zao. Siku hizi unaweza ukaona simu ambayo ina vibonyezo vichache au haina kabisa. Ulimwengu wa zile skrini za kutachi umetuteka kabisa, je tupo tayari kujikwamua katika hili? jibu ni hapana kwa sababu tunapenda hali hii!

teknokona_iphone6

Pengine Baada Ya Hizi na Zile Za 6s na 6s Plus Tusitegemee Kitufe Hichi Cha Kuturudisha Nyumbani

Apple walivyoleta kitufe cha nyumbani katika iPhone walirahisisha matumizi mazima ya simu zao kwa watuamiaji wao. Inakuwa ni rahisi kutumia simu hii ikiwa na kibonyezo kimoja. Kibonyezo hiki sifa yake kubwa ni kuwa ‘Hata kama upo sehemu yeyote, ukikibonyeza tuu kitakupeleka nyumbani’ chukulia hali hii kama vile umepotea na hicho ndicho pekee kinachokupeleka kwenu.

mapinduzi haya yalitokea baada ya simu zingine kama vile blackberry na Nokia kuonekana zina vibonyezo vingi ambavyo mtumiaji alilazimika kuvitumia ile kuenda sehemu tofauti tofauti katika simu yake. Yalikua ni mapinduzi makubwa lakini cha kushangaza ni bado kitufe hicho kimebaki kuwa ni cha aina yake.

SOMA PIA  Ni Rahisi Kwa App Za Magemu Kupata Nafasi Za Juu Kuliko App Zingine Huko App Store! #2022

Tokea simu mpya za  iPhone 6s Plus na iPhone 6s ziiingie sokoni inasemekana iPhone mpya zitakazotengenezwa baada ya hizi zitakuwa na vitufe vichache na hii inawezekana ikawa ni kuondolewa kwa kile kitufe cha nyumbani (home button).

iphone 6S Rangi

Mengi Yatabadilika Usishangae Na Rangi Kuwa Moja Kati Ya Mambo hayo.

Pengine labda kampuni (Apple) likifanya hivi (kuondoa kitufe hicho) litapata uwanja mkubwa wa kuweka skrini, Yaani skrini itakua ni kubwa sana (kuanzia kule juu mpaka eneo zima la kitufe cha nyumbani)

SOMA PIA  Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa-Namba 10 hadi 1

Hii inamaanisha kuwa kampuni la Apple wanaweza wakaleta simu zenye skrini kubwa kuliko hizi za sasa lakini pia zikawa na ukubwa kama huu wa sasa tuu. mabadiliko yunaweza kuwa katika skrini tuu au yakawa ni zaidi ya hapo.

Mabadiliko yanaweza yakawa ni mengi tuu zaidi ya haya kutoka Apple, sema hili ndio linalotegemewa kwa kiasi kikubwa. Tuambie sehemu ya comment unaonaje swala hili, kuodolewa kwa kile kitufe kutaleta mapinduzi au kampuni litapoteza umaarufu wake kwa kuondoa kitufe kinachowatofautisha na makampuni mengine. Tembelea mtandao wako pendwa kila siku wa TeknoKona. TeknoKona Tupo Pamoja Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania