fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti simu Tanzania Teknolojia

Zifahamu Huduma Mpya Kutoka Airtel – Wifi na Kadi ya Premier

Zifahamu Huduma Mpya Kutoka Airtel – Wifi na Kadi ya Premier

Spread the love

Airtel-PremierWikiendi iliyopita Airtel wametambulisha huduma mbili kubwa nazo ni kadi ya ‘premier’ kwa wateja wake pamoja na kifaa cha huduma ya WiFI kwa ajili ya manyumbani.

Je hutegemee nini katika huduma hizi? Tupo hapa kujibu swali hilo.

Huduma ya kadi ya Airtel Premier itawapatia wateja wakubwa wa mtandao huo nafasi za punguzo la gharama (discounts) katika maeneo mbalimbali kama maduka na pia itawapatia wateja hao nafasi ya kujivinjari katika maeneo spesheli (lounges) katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani (kwa makadirio ni zaidi ya viwanja 700 ulimwenguni kote).

SOMA PIA  Programu ya usaidizi kutoka Google kutanua wigo wake

Waziri Dk Mary Nagu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu amesifia hatua hiyo akidai Airtel imefanya jambo zuri katika kusaidia ukuaji wa biashara, na mahusiano ya kibiashara.

Airtel Family WiFi – Huduma ya intaneti ya WiFi kwa ajili ya familia. Maarufu kama mobile WiFi, Airtel wameleta kifaa kidogo ambacho utaweza kuweka laini yako na kujiunga bando ya intaneti na kuweza kuitumia kwa vifaa zaidi ya kimoja. Hii itasaidia kupunguza gharama za huduma ya intaneti majumbani kwa kiasi flani.

SOMA PIA  Samsung Galaxy S7 na S7 edge zaendelea kuangaliwa

Vipi, unafikiri unafikiri huduma gani kati ya hizi ni bomba zaidi kwako? Tueleze

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania