Sio wewe tuu unaweza kupiga picha za selfi bali ‘ata watu wa zamani wanaweza’ kupiga picha hizo siku hizi 🙂 . Hivi karibuni mitandao ya kijamii imezongwa na picha za watu wenye miaka mingi sana – Mamia ya miaka. Hii yote ilianza baada ya mbunifu Olivia Muus utembelea katika Nyumba ya sanaa (gallery) huko Copenhagen nchini Denmark kisha akapiga picha ya sanamu marufu katika jumba la sanaa hilo ikiwa inajipiga ‘selfie’ na hapo ndio ‘Museum of selfies’ ilipozaliwa.
“Nilipiga picha kwa kujifurahisha tuu,na nilifurahi kuona hiki kitu kidogo kinavyoweza badilisha sura zao na kuifanya picha nzima kuwa na maana mpya”- alisema Olivia katika blog yake ya tumblr
Katika Twitter na Instagram watu wamekuwa wakituma picha za sanamu mbali mbali zikiwa zinapiga ‘selfie’ kwa kutumia alama ya reli (hashtag) ya #museumofselfies na zimekuwa zikivutia sana. ushawahi kukaa na kufikiria sanamu la mtu wa kale linajifotoa ‘selfie’? hebu pata picha kwanza!
Ushapata picha sio! Ni kale kamchezo flani ka mtandaoni ambako kanahushisha picha sanasana katika mtandao wa instagram. kwa picha nyingi zaidi bofya hapa
Kila mtu anaweza piga hizi ‘selfies’, ningependa kuona kila mtu anajaribu. Lakini kabla ya kupiga picha hizo hakikisha una kibali kinacho kuruhusu kupiga pia usitumie flashi ya kamera yako. Kama ukipiga yako tu ‘tag’ katika akaunti yetu ya instagram hapa. Sasa Hata Sanamu Zinapiga Selfies, piga picha za sanamu au michoro ya watu wa miaka mingi iliyopita na ambatanisha na hashtagi ya #MuseumOfSelfies
Siku Njema!!
No Comment! Be the first one.