fbpx

Jinsi ya kutatua tatizo la “Download pending” kwenye Playstore. #Maujanja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu janja (rununu) tunazotumia hasa kwa wale tunaotumia simu za Android tunakumbana na matatizo mengi lakini ambalo tunakutananalo ni “Download pending” pale unapojaribu kupakua/kufanya masasisho ya programu tumishi.

Unaweza ukafikri kuwa umeishiwa na kifurushi cha intaneti na ndio maana ukijaribu kushusha kitu kutoka kwenye soko la programu tumishi za Android maarufu kama Playstore inakataa huku bado ukiwa na salio la kutosha.

Download pending” ni tatizo ambalo linatokana na kuwepo kwa nafasi finyu ya Playstore kuweza kukubali data za programu tumishi nyingine.

Download pending

“Cache Data” zikibaki kwenye simu zinaweza kuchukua nafasi ya hata GB 1 na zaidi.

Jinsi ya kutatua tatizo la “Download Pending” kwenye simu za Android.

Tatizo hilo unaweza ukafikiri kuwa ni vigumu sana kuondoa lakini la hasha! Unatakiwa kufanya kitu kidogo tu; ingia settings>>apps>>Google Playstore>>App info kisha bofya “Clear Data“.

Download pending

Namna ya kuondokana na tatizo la “Download pending” kwenye simu za Android.

Kwa ujumla ni muhimu sana kuhakikisha unaondoa “Cache data” kwenye simu yako kama njia/mbinu ya kuongeza nafasi ndani ya rununu.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ushirikiano kati ya HaloPesa na VISA wazinduliwa
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.