fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps simu Tablet

Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo

Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo

Spread the love

clean-androidKuna muda mwingi simu zinakuwaga nzito na utendaji wake wa kazi unaathirika sana, zinakuwa na joto sana na muda mwingine ata zinaweza zikawa ata zinazima pale chaji ikiwa safi tuu. Na hapa ndio app hii ya Clean Master inakuja.

Ata pale unapokuta nafasi ya uhifadhi (storage) imepungua kwenye simu au tableti yako ya Android, Clean Master itakuonesha ni nini hasa kinakula nafasi na kukusaidia kufuta vitu usivyoitaji.

Utakapofungua app ya Clean Master itakuonesha kupitia michoro (graphs) ni nini kina kula nafasi kwenye simu au memori kadi yako. Pia itakuonesha ata nafasi inayoshikiliwa uchafu (cache) uliotokana na oparesheni za apps ulizonazo. Kupitia chaguo rahisi la ‘Clean’ yaani safisha, app inasaidia sana kwani hauitaji kuwa na ujuzi mwingi sana, katika utumiaji wa app hii kwa muda mrefu haijawahi kuharibu au kuathiri app au mafaili yeyote muhimu.

SOMA PIA  Qualcomm Kuja Na Simu Janja Yake Kwa Ushirika Wa Asus!

Ata pale simu inapokuwa inaanza kushika joto app hii itakuonesha ni apps gani zinasababisha joto hilo, na inakupa chaguo la kuzifunga apps hizo.

cleanmaster

Kwa kiasi kikubwa app hii itasaidia kuongeza maisha ya simu yako. Kushusha bofya hapa – Google Play

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] Ingawa vipengele hivi ni huru na vya wazi kabisa kwenye androidi kuongeza kasi ya simu yako na kuokoa uhifadhi, zipo app ambazo zinakupa urahisi wa kutumia ujanja huu automatiki – yani bila wewe kuwa na haja ya kutumia muda mwingi kubonyezabonyeza simu yako. App hii ni kama CleanMaster ambayo tumewahi kuielezea -> Ifahamu app ya Clean Master […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania