Watu wengi hutumia kompyuta za umma japo kwa mara moja moja na wengi hawafahamu hatari za kutumia komyuta hizo. Katika ulimwengu ambao makampuni ya teknolojia yanafanya mambo mengi kufanya mambo ya mtandaoni kuwa ya kibanfsi zaidi, inakuwa rahisi sana kwa mtu kuibiwa taarifa za muhimu. Pia, kompyuta za umma ni hatari sana kwa kusambaza virusi.
Kuanika Taarifa zako Muhimu:
Kuna uzembe unaotokea kwa watumiaji wa kompyuta za umma kwa kuacha taarifa za akaunti ya barua-pepe na mitandao ya jamii wazi wanapotoka kwenye kompyuta hizo. Haitoshi kufunga kivinjari wavuti, mitandao ya siku hizi hupendelea zaidi kuhifadhi taarifa zako kwenye kompyuta kurahisha matumizi na hivyo kukuweka kwenye hatari zaidi.
Wizi wa Nenosiri (Password) na Akaunti za Benki
Siku hizi, wahalifu wa kompyuta (mahaka) hutumia programu maalumu ziitwazo ‘Key-logger’ kuiba nenosiri, akaunti za benki na taarifa nyingine muhimu za watu kwenye kompyuta za umma. Programu hizo hurekodi kila kitu unachobonyeza kwenye kibodi na kuhifadhi au kutuma kwa mhalifu. Key-logger zinapatikana bure na kirahisi kwenye intaneti kwa sababu zilitengenezwa kutumika na wazazi kufuatilia mienendo ya watoto kwenye kompyuta. Mtu yeyote anaweza kuzipata na kufanya uhalifu.
Virusi vya Simu/ Kompyuta
Mbali na kuibiwa taarifa muhimu, kompyuta za umma pia huongoza kwa kusambaza virusi vya kidijitali. Wengi wetu tunajiamini kutumia simu kwenye kompyuta za steshenari na makafee bila wasiwasi. Simu au kifaa kingine kina nafasi kubwa ya kupata virusi kutoka kompyuta hizi na kuna nafasi kubwa tutahamishia kwenye kompyuta nyingine.
Ufanye Nini?
Kiukweli, kuna kanuni moja tu linapokuja suala la kutumia kompyuta za umma – Usifungue akanunti zako muhimu ikiwemo taarifa za benki. Zaidi ya hapo, chunguza ujuzi wa ‘admin’ wa kompyuta kama ana mamlaka kamili na ujuzi wa ndani wa usalama wa kompyuta na usihifadhi data yoyote kwenye kompyuta za umma, hasa nyaraka muhimu. Kama umezipakua mtandaoni, zifute na hakikisha hazipo kwenye ‘recycle bin’. Hautataka mtu azikute na kuweza kuzitumia vibaya.
Kama inabidi kutumia kivinjari-wavuti, tumia kivinjari-wavuti cha kisasa na ingia ‘Private Browsing’, chaguzo amabayo haihifadhi data zako. ‘Log Out’, yani toka kwenye akaunti kabla ya kufunga kivinjari-wavuti. Badilisha nenosiri yako mara kwa mara kukunusuru kama kuna mtu ameidaka. Futa kabisa historia yako kwenye kivinjari wavuti kwa kubonyeza ctrl + shift + delete na kuchagua kufuta kila kitu, wakati unapomaliza kazi zako.
No Comment! Be the first one.