Microsoft wamesema tujiandae kwa ujio wa toleo la Microsoft Office 2021 kwa kompyuta za Windows na MacOS. Toleo hilo litakuja baadae mwaka huu.
Programu ya Microsoft Office ni programu maarufu inayowasaidia watumiaji kutengeneza dokumenti za aina mbalimbali kupitia programu za Word, Excel, Powerpoint na nyingine zinazokuja kwa pamoja kupitia programu hii.
Ingawa kwa miaka kadhaa Microsoft wamekuwa wakitumia nguvu sana katika kuongeza watumiaji wa toleo la mtandaoni la Microsoft Office linaloenda kwa jina la Office 365 ambalo ni malipo ya kila mwezi bado wanatambua kuna wengi ambao wanataka toleo lililozoeleka la kununua programu ya kompyuta kwa kuilipia mara moja tuu.
Microsoft bado hawajasema vipya gani vinakuja kwenye toleo hili ila moja ya kitu ambacho tayari kishawekwa wazi ni uwezo wa programu hiyo kuwa katika dark mode. Fahamu zaidi kuhusu Dark Mode na kuiwezesha kwenye Windows 10 kwa kubofya hapa – Kuwezesha Windows 10 Dark Mode

Microsoft wamesema kwa toleo hili la Microsoft Office baada ya kununua mtumiaji ataweza kupata updates/masasisho kwa kipindi cha miaka mitano, hii ni chini ukilinganisha na toleo lililopita ambalo lilipata masasisho kwa miaka 7.
Bado hawajaweka tarehe rasmi, ila tunategemea habari zaidi zitatoka hapo mbeleni watakapokaribia kuliachia toleo hilo sokoni.
Vyanzo: USATODAY na vyanzo mbalimbali
No Comment! Be the first one.