fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Android apps Maujanja

#Maujanja – Tatua tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store – Error 505

#Maujanja – Tatua tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store – Error 505

tecno

Kuna matatizo mengine unayoweza kukutana nayo katika simu janja yako yakakulazimisha hadi uformat simu lakini kumbe kuna kanjia kadogo tuu ungetumia na ungetatua tatizo lako kabisa.

error 505

Tatizo la error 505 katika app ya Google Play Store

Leo fahamu jinsi ya kutatua tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store huku ikukupa neno ‘Error 505’.

Tatizo la Google Play Store Error 505 linaweza tatuliwa kwa kutumia njia zifuatazo;

Ya kwanza: Zima, washa pia hakikisha muda wa saa

Zima na kuwasha simu yako. Muda mwingine kufanya hili tuu kunaweza ondoa tatizo hili na utaweza kupakua apps bila shida tena. Na pia hakikisha kama saa ya simu yako inaonesha muda ulio sahihi.

Jaribu kupakua app yeyote tena kupitia Google Play Store, ikikupa error ile ile tena nenda jaribu njia ya pili.

Ya pili: Cache na Data za Google Play Store

Futa Cache na Data za Google Play Store

  • Nenda Settings
  • Bofya Apps au kwenye simu nyingine huwa panaitwa Application Manager
  • Bofya ‘All’ katika eneo la juu
  • Tafuta Google Play Store katika orodha na kisha ibofye
  • Hapa utaona machaguo mawili ‘Clear Cache’ na ‘Clear Data’, Bofya Clear Data kisha Clear Cache
SOMA PIA  Dondoo za Ulinzi na Usalama wa Pesa na Huduma za Kibenki ktk Simu Yako

Njia ya tatu: Akaunti ya Google

  • Nenda Settings
  • Katika eneo la Accounts bofya Google
  • Bofya kwenye akaunti yako ya Google na kisha bofya ‘Remove Account’
  • Zima simu yako na waishe tena
  • Fuata hatua za kuweka akaunti ya Google upya

Kama njia zote hizo zimeshindikana basi hapa ndio itabidi ufunye maamuzi mazito. Ureset simu yako, kuhusu hili soma – Jinsi ya kureset au kuformat simu ya Android

SOMA PIA  Tegemea Kuweza Kutumia Apps za Android kwenye Kompyuta

Ni matumaini yetu makala hii imekusaidia.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania