Je umekuwa unatafuta njia ya kuangalia video za YouTube isiyokula data sana? Basi app ya YouTube Go inaweza ikawa ndio jibu sahihi.

YouTube GO ni nini?
YouTube GO ni app kutoka Google inayokuwezesha kutazama video mbalimbali za YouTube bila utumiaji mkubwa wa data na ata maeneo ambayo huduma ya intaneti haina nguvu sana (kimombo – slow).
YouTube Go imetengenezwa kutoka toleo la kawaida la YouTube la simu za Android ila hili limepunguzwa ukubwa na majonjo mengine mbalimbali ambayo mtumiaji wa kawaida wa kwenye maeneo yasiyokuwa na intaneti ya kasi haoni maana yake.
SOMA PIA Sio ndani dakika 7 tu! Unaweza kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika WhatsApp #Maujanja
YouTube Go inaruhusu watumiaji wake kuruhusu video ya YouTube kujihafadhi ndani ya app hiyo na hivyo kuweza kutazamwa tena ata kama mtu hatokuwa na huduma ya intaneti kwa kipindi hicho.