fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Huawei Oppo simu Xiaomi

Apple washika namba moja kimauzo robo ya mwisho ya 2020, Huawei waporomoka sana

Apple washika namba moja kimauzo robo ya mwisho ya 2020, Huawei waporomoka sana

Apple washika namba moja kimauzo katika sekta ya simu janja katika robo ya mwisho ya mwaka 2020. Hii ni kutokana na data mpya za kimasoko kutoka shirika la Gartner.

Hii ni mara ya kwanza tokeo mwaka 2016 kwa kampuni ya Apple kuweza kushika nafasi ya kwanza kwa kuipiku Samsung, kwa muda mrefu Samsung amekuwa akikamata nafasi ya kwanza ya kimauzo ya kila kipindi cha miezi mitatu cha mauzo.

Uingizaji sokoni wa simu zao mpya za iPhone 12 na punguzo la bei kwa baadhi ya matoleo ya nyuma umeifanya robo hiyo ya mwezi Oktoba hadi Disemba 2020 kuwa ya kimafanikio kwa Apple.

apple washika namba moja

Matoleo mapya, iPhone 12 pamoja na kushuka kwa bei ya matoleo ya nyuma kumesaidia

 

Idadi ni katika maelfu, ‘000

Muuzaji Mauzo ya robo ya nne 2020

(Okt-Dec 2020)

Asilimia ya ushikaji soko (Okt-Dec 2020) (%) Mauzo ya robo ya nne 2019

(Okt-Dec 2019)

Asilimia ya ushikaji soko (Okt-Dec 2019) (%) Ukuaji – mlinganisho wa Okt-Dec 2020 vs Okt-Dec 2019 (%)
Apple 79,942.7 20.8 69,550.6 17.1 14.9
Samsung 62,117.0 16.2 70,404.4 17.3 -11.8
Xiaomi 43,430.3 11.3 32,446.9 8.0 33.9
OPPO 34,373.7 8.9 30,452.5 7.5 12.9
Huawei 34,315.7 8.9 58,301.6 14.3 -41.1
Wengine 130,442.8 33.9 145,482.1 35.8 -10.3
Jumla 384,622.3 100.0 406,638.1 100.0 -5.4

Simu za Apple zilichukua asilimia 20.8 ya simu janja zote zilizouzika, nafasi ya pili ikienda kwa Samsung kwa asilimia 16.2, nafasi ya tatu imechukuliwa na kampuni ya Xiaomi ambaye alichukua asilimia 11.3. Oppo ameweza pia kuipika Huawei, ambapo Oppo wanachukua nafasi ya nne kwa asilimia 8.9, huku Huawei wakichukua nafasi ya tano nao kwa asilimia 8.9 ila wakiwa na tofauti ndogo ya kimauzo ukilinganisha na Oppo.

Makampuni mengine nje ya haya matano yaliwakilisha asilimia 33.9 ya simu zote zilizouzwa. Kwa ujumla wake simu janja 384,622 ziliuzwa katika kipindi hicho.

Ukilinganisha na mauzo ya simu janja ya mwaka 2019 katika robo ya mwisho ya mwaka, Huawei wameporomoka kimauzo kwa zaidi ya asilimia 41, hali hii ikichangiwa na vikwazo vya kibiashara walivyowekewa na Marekani. Katika kipindi hicho hicho mauzo ya Xiaomi yamekuwa kwa zaidi ya asilimia 33.9, wakati ya Samsung yakiporomoka kwa asilimia 11.8.

Kwa kipindi kizima cha mwaka jana bado Samsung inashika nafasi ya kwanza, kwa asilimia 18.8, Apple nafasi ya pili kwa asilimia 14.8, Huawei nafasi ya tatu kwa asilimia 13.5, Xiaomi nafasi ya nne kwa asilimia 10.8 na Oppo nafasi ya tano kwa asilimia 8.3 na huku makampuni mengine yakichukua asilimia 33.7. Hii ni kutoka kwenye idadi ya mauzi ya simu janja milioni 1,347,869. Kwa ujumla mauzo ya simu janja yaliporomoka kwa asilimia 12.5 ukilinganisha na idadi ya mauzo ya mwaka 2019.

Xiaomi wanakua kwa kasi zaidi kuliko wengine wote.

Idadi ni katika maelfu, ‘000

Mtengenezaji 2020

Mauzo

2020

Umiliki wa soko (%)

2019

Mauzo

2019

Umiliki wa soko (%)

2020-2019

Ukuaji (%)

Samsung 253,025.0 18.8 296,194.0 19.2 -14.6
Apple 199,847.3 14.8 193,475.1 12.6 3.3
Huawei 182,610.2 13.5 240,615.5 15.6 -24.1
Xiaomi 145,802.7 10.8 126,049.2 8.2 15.7
OPPO 111,785.2 8.3 118,693.2 7.7 -5.8
Wengine 454,799.4 33.7 565,630.0 36.7 -19.6
Jumla 1,347,869.8 100.0 1,540,657.0 100.0 -12.5

Data za kiujumla zinaonesha katika makampuni yote ya simu ni Xiaomi ndiye anayekuza mauzo yake kwa kasi zaidi. Ingawa 2020 ulikuwa mwaka mbaya kimauzo kwa karibia wote, Xiaomi waliweza kukuza mauzo yao kwa asilimia 15.7 ukilinganisha na mwaka 2019. Apple katika kipindi hicho alikuwa mauzo kwa asilimia 3.3 tu, huku Samsung yakiporomoka kwa asilimia 14.6, Huawei nao mauzo yakiporomoka kwa asilimia 24.1, Oppo yakiporomoka kwa asilimia 5.8 na watengenezaji wengine yakiporomoka kwa wastani wa asilimia 19.6.

Mwaka 2021 utakuja kutuonesha ni kwa jinsi gani hali ya ushindani inabadilika katika makampuni ya utengenezaji simu janja. Kuna uwezekano mkubwa kampuni ya Xiaomi ikaja kufanikiwa kupigania nafasi mbili za juu kutoka kwa Samsung au Apple.

Chanzo: Gartner

SOMA PIA  JIHUDUMIE: Huduma mpya kubatilisha muamala
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania