Mara kadhaa kwenye makala zangu nimekuwa nikisema Xiaomi Corporation ni kampuni ambayo inakuwa kwa kasi sana na hii inadhihirika kwa bidhaa zake ambazo tayari zimeshaingia sokoni kama Mi 11 Ultra lakini hata zile ambazo zimeshazinduliwa tu bila kusahau zilizopo “Jikoni”.
Tangu mwaka 2020, ilionekana kuwa ni hatamu ya teknolojia ya 5G na bado inaendelea kwani makampuni makubwa yanayofanya vizuri kwenye soko la ushindani yamekuwa yakihakikisha yanatoa simu janja za kisasa zinazoendana na soko linataka nini. Hivi karibuni Xiaomi Mi 11 Ultra ilizinduliwa na mwezi Aprili ikaingia sokoni. Kiukweli ni simu nzuri ya kuvutia na yenye mengi ambayo yanafanya watu waiongelee rununu hii. Pata kufahamu sifa na udani wa Xiaomi Mi 11 Ultra kama ifuatavyo:-
- Ukubwa: inchi 6.81 (1440×3200 px)
- Ubora: AMOLED, ung’avu wa hali ya juu sana/Gorilla Glass Victus kwa mbele+imezungukwa na alminium-uso wa nyuma
- Diski uhifadhi: GB 256 na 512 GB
- RAM: 8 GB na GB 12
- Kamera Kuu: MP 50, MP 48 na MP 48+taa mbili za kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
- Kamera ya Mbele: MP 20
- Li-Ion 5000 mAh,
- USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 67W (100% kwa dakika 36 na kufika 100% kwa teknolojia ya kuchaji bila waya inachukua dakika 39)
- Snapdragon 888 5G
- Gramu 234
Programu Endeshi
- MIUI 12.5, Android 11
- Nyeusi na Nyeupe
- Bei yake ni kati ya $1,099 (zaidi ya Tsh. 2,527,700) na $1,599 (zaidi ya Tsh. 3,677,700) kwa ughaibuni
Mabaya na mazuri ya Xiaomi Mi 11 Ultra
Kwa ujumla wake rununu hii ina mengi mazuri yanayoifanya iwe ni ya kuvutia kwa aina yake na vivutio vyenyewe vipo kwenye uwezo wa betri, kioo, ufanisi, kamera, muundo na teknolojia ya kuchaji haraka. Mabaya kwenye hii simu janja ni ghali, nzito, ubora wa kamera ya mbele si wa kuvutia kiasi hicho na hawajaweka wazi iwapo simu hii itapokea masasisho ya programu endeshi huko mbeleni.
TeknoKona tumeshafanya kazi yetu na huo ndio undani ambao unatosha kuweza kutathimini iwapo inafaa kuwepo kwenye mipango yako ya kuweza kuinunua au la!.
Vyanzo: Android Authority, GSMArena
nimesha iwekea order iko njiani
Hongera yako ndugu yangu.