Pengine labda unajua ni kipi bora kuliko vyote mpaka sasa, lakini ni vyema kujua vingine pia. Katika kifaa chako cha Android wewe unatumia kivinjari kipi?
Je hiko unachotumia ndio bora kuliko vingine? Leo TeknoKona kama kawaida yetu tunataka kukupatia vile vitano (5) bora zaidi. Kama unatumia moja kati ya hivi basi wewe ni mjanja
Tuvijue Vivinjari 5 Bora Zaidi.
1. Chrome

Hiki ndio kivinjari kilichokuja kuvunja rekodi ya kivinjari cha ‘Internet Explorer’ kutoka katika kampuni la Microsoft. Kivinjari hiki ambacho kinamilikiwa na kampuni la Google kimejipatia umaarufu wake kwani kina vipengele vingi ndani yake. Vipengele hivyo kwa namna moja ua nyingine vinamuwezesha mtumiaji wa mtandao kuperuzi kwa urahisi zaidi.
Utafurahia kutumia kivinjari hichi cha chrome zaidi kama una akaunti ya Google. Baada ya kuingiza akaunti yako unaweza ukafanya mambo mengi zaidi kama vile kuhifadhi baadhi ya kurasa (bookmark). Pia unaweza ukaperuzi katika kurasa kwa siri kwa kutumia ule mfumo wa ‘incognito’. Ukiachana na hilo kuna mambo mengine mengi. Ili kujionea unaweza ukashasha kivinjari hicho hapa
2. Opera

Watumaiji wengi wa simu huwa wanatumia kivinjari cha opera. Kwa kifupi kivinjari hiki kana watumiaji wengi wa simu kuliko wale wa kompyuta. Kabla ya chrome hiki kilikua ni moja ya kivinjari maarufu sana – bado ni maarufu – duniani
Kama kama chrome kilivyo hata hiki pia kinaweza ukaingia katika baadhi ya kurasa kwa siri (incognito). Pia kama ukiwa na akaunti ya opera unaweza ingia kwa kutumia akaunti hiyo na hapo unaweza ukahifadhi kurasa n.k. Sifa kubwa ya kivinjari hiki ni ulaji mdogo wa data za mtandao
Mara yako ya mwisho kutumia Opera ni lini, Au bado unaendelea kuitumia? Unaweza ukakipakua hapa
3. FireFox

Moja kati ya vivinjari vya mwanzo mwanzo kabisa, nakumbuka kuna kipindi ulikuwa huniambii kitu kuhusiana na kivinjari hiki. Lakini teknolojia inabadilika – mambo yanabadilika – na vitu vingine vyenye ubora zaidi vinaingia sokoni. Tuachane na hayo, Mozila FireFox ni kivinjari kilicho anzishwa mwaka 2002 lakini kutumika katika vifaa vya Android kumeanzia mwaka 2012. Mambo mengine mengi kivinjari hiki kinavyofanya ni kama vivinjari vingine tuu. Kukishusha katika simu yako ya Android ingia hapa
4. Puffin

Hiki sio maarufu sana kama ukilinganisha na vivinjari vingine lakini haimaanishi kuwa sio kizuri. Pia kivinajari cha Puffin kina uwezo wa kuingia mtandaoni kwa siri, ulaji mdogo wa data katika mtandao n.k. Kinachotofauti hichi na vingine ni sapoti yake kwa sehemu/kurasa zinazohitaji Adobe flash na vitu kama vile utendaji mzuri wa kazi wakati una ‘stream’ mafaili katika simu yako. Ili kukishusha unatakiwa kuingia hapa
5. Dolphin

Kivinjari hiki kinaweza kufanya mambo mengi kama vile kutafuta/kuingia katika kurasa kwa kutumia sauti (bila kuandika) mfano unaweza ukasema ‘Open Google.com’ na kivinjari kikafungua kurasa hiyo. Pia unaweza ukakiamuru kivinjari kifungue ukurasa Fulani baada yaw ewe kuchora alama Fulani. Mambo mengine ambayo kivinjari hiki kinaweza kufanya ni kama yale ambayo yanaweza fanyika katika vivinjari vingine kama vile kuingia katika kurasa kwa siri n.k. Kukishusha katika simu yako ya Android ingia hapa
NYONGEZA: Hiki sio kivinjari kingine bali ni UC Browser

Wengi (wasomaji wetu) wanakipenda na nimeona ntakuwa nawakatili nisipokiweka. Kwa haraka haraka UC Browser ni kivinjari cha aina yake, moja kati ya sifa zake ni kwamba kinakula data kidogo za mtandao wakati unaperuzi. Mambo mengine ambayo yaweza kufanyika katika UC Browser yanafanana na vivinjari vingine. Kama unataka kukishusha katika simu yako ya Android ingia hapa