fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Teknolojia Xiaomi

Ifahamu Xiaomi Redmi 9A

Ifahamu Xiaomi Redmi 9A

Xiaomi Redmi 9A ni simu janja ambayo hivi karibuni tuu ilitokea kwenye orodha ya rununu ambazo zilifanya vizuri kimauzo mwezi Januari 2021. Je, unafahamu sifa zake?

Xiaomi Corporation ni kampuni ambayo inakuwa kwa kasi sana na yenye makao yake makuu huko Beijing-Uchina ambapo ilianzishwa mwezi Aprili mwaka 2010 na katika kipindi kifupi tuu bidhaa zake zimeweza kupenya maeneo mengi duniani na kuuzika kiasi cha kuwa miongoni mwa kampuni zinazofanya vizuri kimauzo katika miaka ya karibuni.

SOMA PIA  Microsoft kuja na simu zinazojua unapotaka kubonyeza kabla ya wewe kufanya hivyo

Xiaomi Corporation ina bidhaa nyingi tuu sokoni na mojawapo kati ya hizo ni Redmi 9A ambayo ilizinduliwa Juni, 30 2020 na kuingia sokoni Julai 7. Ni simu janja iliyonipa shauku ya kutaka kujua ina sifa gani hasa za kuifanya kuwa miongoni mwa zile zilizofanya vizuri kimauzo mwezi Januari 2021? Niseme tuu fuata nami mpaka mwisho wa makala hii. Tuanze na:

Memori :
 • Diski uhifadhi: GB 32, GB 64 na 128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka GB 512
 • RAM: 2GB, 3GB, GB 4 na GB 6
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 13+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
 • Kamera ya Mbele: MP 5
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 10W
Kipuri mama :
 • MediaTek Helio G25
Uzito :
 • Gramu 196

Programu Endeshi

 • MIUI 12, Android 10
Rangi/Bei :
 • KijaniKahawia na Bluu
 • Kwa bei ya chini kabisa kwa maana yenye 2G/32G inaweza kuanzia Tsh. 250,000 kwa Tanzania. Bei inaweza kubadilika kulingana na muuzaji mwenyewe.
  Redmi 9A

  Xiaomi Redmi 9A ina teknolojia ya kutambua sura kama njia ulinzi, Wi-Fi, redio, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni, Bluetooth 5.0, 3G/4G, inatumia kadi mbili za simu.

   

Ukizungumzia muonekano, ubora wa betri, memori na bila kusahau bei yake kuwa inayohimilika naamini ndio vitu vilivyochagiza kuweza kufanya vizuri sokoni na kuifanya kampuni husika kuendelea kung’ara kwenye soko la ushindani. Je, una mawazo tufauti? Tuangependa kusikia kutoka kwako.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360 na mitandao mbalimbali

SOMA PIA  iWatch : Apple na Saa ya Milioni 18+
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania