Tigo na Zantel Tanzania ni kampuni za mawasiliano ambazo zimekuwa zikifanya kazi kwa miaka mingi tuu na kuweza kufikia wateja mijini na vijijini lakini pia visiwani Zanzibar.
Tigo Tanzania ni moja ya kampuni ya mawasiliano yenye wateja wengi (ya pili baada ya Vodacom Tanzania) ambayo imekuwa ikitoa huduma tangu mwaka 1995 hadi sasa huku mmiliki mkuu akiwa Millicom International. Zantel imekuwa nchini ya mwamvuli wa Tigo Tanzania tangu Novemba 4 2019 ambapo muunganilko huo haukuathiri wateja wa kampuni husika na hivyo utoaji wa huduma umeendelea kama kawaida hadi sasa.
Taarifa iliyotoka leo imeweka wazi kuwa Tigo na Zantel Tanzania zitakuwa chini ya wamiliki wapya kwa maana ya hisa zote za kampuni hizo zitamilikiwa na Axian Group. Millicom International inaagana na soko la Afrika ambalo amedumu kwa zaidi ya miaka 25 hivyo kupeleka nguvu zaidi Amerika Kusini.
Ifahamu kidogo Axian Group
Hii ni kampuni ya mawasilaino yenye makao yake Makuu Antananarivo-Madagascar. Huduma zake kwa sasa zinapatikana nchini Madagascar, Senegal, Togo, visiwa vya Reunion, Mayotte pamoja na Comoro. Axian Group wamepanga kuwekeza nchini Tanzania kwenye huduma za mawasiliano $400 milioni katika kipidi cha miaka mitano ambapo watafanya yafuatayo:-
- kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ili kuongeza ushindani, kuboresha uendeshaji pamoja na kuhakikisha mageuzi ya uchumi wa kidijitali,
- kuhimiza ukuaji wa taaluma kwa wafanyakazi kupitia mafunzo ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na
- Kuchochea ujumuishwaji wa watu kiuchumi pamoja na kuongeza ubunifu kwenye huduma za kifedha.
Je, wajua?
- Mpaka Disemba 2020, Tigo Tanzania ndio kampuni ya pili kuhudumia wateja wengi zaidi baada ya Vodacom,
- Huduma ya TigoPesa ilianzishwa mwaka 2010 na
- Aprili 2014, Tigo Tanzania ilizindua kasi ya mawasiliano kwa 4G jijini Dar es Salaam na hadi kufikia mwaka 2016 huduma hiyo ilikuwa imeshaenea Tanzania nzima.
Millicom International wamewahakikishia wateja wao kuwa huduma zao kuwa zitaendelea kama zilivyo mpaka watakapopata uthibitisho kutoka mamlaka za usimamizi. Je, unaizungumziaje taarifa hii?
Vyanzo: Gazeti la Mwananchi, Tovuti ya Zantel Tanzania
No Comment! Be the first one.