fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Sifa za ndani kuhusu Samsung Galaxy M62

Sifa za ndani kuhusu Samsung Galaxy M62

Samsung ina wateja wengi tuu duniani kote na hii inatokana na ubora wa bidhaa zao mbalimbali bila kusahau zile ambazo zinarahisisha mawasiliano katika ulimwengu huu uliotawaliwa na teknolojia.

Leo, Februari 24 2021 kupitia tovuti rasmi Samsung nchini Thailand zimeorodheshwa sifa za simu janja ambayo itatoka mwamzoni mwa mwezi Machi ambapo ndipo Samsung Galaxy M62 italetwa machoni pa watu. Je, simu hiyo ina sifa gani? Soma makala hii hadi mwisho.Galaxy M62

SOMA PIA  Kuingia sokoni kwa BlackBerry Evolve

Sifa zake ni zipi?

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.7
 • Ubora: Super AMOLED ya 1080 pixels
Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB/256GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
 • RAM: 6GB/8GB
Kamera :
 • Kamera Kuu: Megapixel 64, 12 na 5
 • Kamera ya Selfi: Megapixel 32
Kipuri mama :
 • Exynos 9825
Rangi :
 • Kijani, Bluu na Kawawia

  Galaxy M62

  Nguvu ya betri kwenye Samsung Galaxy M62.

Mengi zaidi kuhusu Samsung Galaxy M62 yataweza kufahamika Machi, 3 2021 ambapo ndipo itakapozinduliwa rasmi na kama kawaida yetu TeknoKona tutaendelea kuwahabarisha kadri tutakavyokuwa tunapata taarifa.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

SOMA PIA  Kutumia teknolojia ya Hololens: Sayari ya Mars 'kuja' Duniani
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania