fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Teknolojia

Kipini cha spika za masikioni ni Teknolojia ya Zaidi ya Miaka 140!

Kipini cha spika za masikioni ni Teknolojia ya Zaidi ya Miaka 140!

Je, una fahamu ya kwamba katika simu janja nyingi moja ya teknolojia ya miaka mingi sana ambayo bado inatumika ni pamoja na ile kipini spika za masikioni yaani ‘Audio jack‘?

Sehemu hiyo kwa ajili ya vifaa vya sauti ni moja ya teknolojia yenye historia ndefu sana. Teknolojia hii ilianza kujipatia uhitaji na umaarufu katika miaka ya 1870 ambapo ilikuwa inatumika katika kuunganisha laini za mawasiliano ya simu katika kipindi ambacho mfumo wa mawasiliano ya simu haukuwa wa moja kwa moja.

SOMA PIA  Samsung Galaxy yenye 5G haipo mbali

Yaani kama unataka kupiga simu kwenda 0754000000 basi ilikubidi upige simu Posta, halafu wao waunganishe laini yako kwenda tundu la waya utakaokuunganisha hadi kwa mtu mwenye namba hiyo. Hivyo, walihitaji mfumo wa uunganishaji waya wa kiurahisi na kiharaka na ambao hautaharibika haraka kutokana na zoezi hilo kufanyika mara kwa mara.

Kipini cha spika

Mchakato wa kufanikisha mawasiliano ya simu kati ya mtu na mtu mwaka 1919.

Kuanzia mawaka 1878, duara lake lilikuwa na ukubwa wa robo inchi (inchi 6.35mm) ila baadae ndio ukapunguzwa ukubwa na kuwa mdogo kwa ya mm 3.5  inaitwa pia “Mini jack”, “Headphone jack” au “TRS jack”, wakati ile kubwa inabeba jina lake la “Audio Jack“.

Kipini cha spika

Kipini cha spika ukubwa wa 3.5mm pamoja na kile cha 6.35mm ambacho hidstoria yake inaanzia mwaka 1878 hadi leo.

Ingawa teknolojia inakuwa lakini bado makampuni mengi wameendelea kushikilia matumizi ya kitu hicho lakini kwa makampuni kama Apple waliona mwaka 2016 ndio tamati ya kipini hicho cha spika za masikioni na kuamua kutumia teknolojia yao wenyewe.

Kipini cha spika

Mbadala wa sehemu ya kuchomeka spika za masikioni kwenye bidhaa za Apple kama simu janja.

Ukuaji wa umaarufu wa headphones za mfumo wa bluetooth unaleta ushindani dhidi ya teknolojia hii. Tayari kuna simu kadhaa zinazokuja bila eneo la audio jack. Ingawa kuna maeneo kama haya matumizi hayo yatapungua ila bado teknolojia hii inaonekana itaendelea kuwepo na kutumika katika matumizi mbalimbali ya kazi za kurekodi na kusikiliza muziki kwa miaka mingi ijayo.

SOMA PIA  WhatsApp: Mambo Ambayo Huenda Huyafahamu

Teknolojia hiyo bado inaonekana kuwa na mashiko kwa kampuni mbalimbali kuendelea kuikumbatia hadi leo. Je, unafikiri teknolojia hiyo bado inafaa?

Chanzo: BBC

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania