fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Hii ndio Samsung Galaxy A02s

Hii ndio Samsung Galaxy A02s

Samsung A02s ambayo iliingia sokoni Jan 04 ya mwaka huu imekuwa ni simu ambayo inawalenga wateja ambao hawapendi mambo mengi yanayohusiana na rununu hivyo kuifanya kuwa simu janja ya bei nafuu.

Wakati simu hii inazinduliwa Nov, 24 2020 nilifurahi kwa kuona rununu nzuri, isiyokuwa na vikorombwezo vingi lakini ambayo imezingatia angalau vile vichache ambavyo ni muhimu katika teknolojia ya leo. Kimsingi Samsung Galaxy A02s na Galaxy A12 zinatofautiana vipengele vichache sana.

SOMA PIA  Barabara ya Sola Yafunguliwa Uholanzi

Sifa za Samsung Galaxy A02s

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.5
 • Ubora: LCD, 720x1600px
Memori :
 • Diski uhifadhi: 32GB/64GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
 • RAM: 3GB na 4GB
Kamera :
 • Kamera Kuu: Megapixel 13, 2, na 2
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 5
Kipuri mama :
 • Qualcomm SDM450 Snapdragon 450

Programu Endeshi

 • Android 10
Rangi/Bei :
 • Bluu, Nyeusi na Nyeupe
 • Bei inaanzia $149 (zaidi ya Tsh. 342,700)
  Galaxy A02s

  Simu hii ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni. Bluetooth 4.2.

   

Unaweza usiwe umevutiwa na simu hii lakini linapokuja kwenye suala utunzaji wa chaji bila ya kujali kama unaperuzi, kuongea na simu la! Basi rununu hii inaweza kuwa kivutio cha wengi ingawa ina mengi ambayo ni sawa na toleo la A12. Tupe neno lako.

Vyanzo: GSMArena, Gizimochina

SOMA PIA  Unafahamu kuwa Google Photos imeboreshwa?
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania