Umeisikia hiyo? Zaidi ya dola laki 7 za kimarekani kwa siku! Wengine wanampenda Kim Kardashian, wengine wanamtamani, wakitamani maisha yake ya kila siku…je wanaweza kufanya mangapi ili kupata ukaribu zaidi wa kuingia katika maisha yake ya usupastaa?
Hapa ndipo watu wakaja na wazo la kutengeneza gemu linaloweza kumpa mtu nafasi ya kuendesha maisha ya Kim Kardashian, gemu la Kim Kardashian: Hollywood lililotengenezwa na kampuni maarufu ya magemu ya GLU Mobile kwa ushirikiano wa karibu na Kim Kardashian mwenyewe linashika chati kwa sasa likiwa linaingiza mapato ya juu kabisa kwa siku, gemu hili ni la bure kushushwa na watu wanaotumia Android au iOS (iPhone na iPad).
Kupitia gemu hili unapata nafasi ya kuendesha maisha ya umaarufu ya Kim Kardashian, ukiwa unamchagulia mavazi ya kuvaa – yawe ya kipekee, kuhakikisha anakutana na mastaa wengine na kwenda kufanya upigwaji picha, kimombo – photo shoot! Vyote ufanyavyo unatakiwa umsaidie apande kutoka kiwango cha ‘E- list’ supastaa hadi afikie ‘A – List’, ambacho ndicho kiwango cha juu cha usupastaa. Na suala la mapato haya linakuja hivi – ukitaka kufanikiwa haraka zaidi inabidi kulipia vitu mbalimbali kama mavazi kutumia pesa za halisi, na hapa ndipo hizo zaidi ya dola 700,000/= kwa siku zinakuja!
Watabiri wa masuala ya mauzo ya magemu wanasema gemu ili likiendelea kufanya vizuri hivi basi hadi mwisho wa Mwaka linaweza likaingiza zaidi ya dola milioni 200 za Marekani! Ndio, yaani ni zaidi ya Tsh 331,700,000,000/=! Upo hapo? Hadi sasa hisa za kampuni ya GLU Mobile zimeanza kufanya vizuri zaidi. Na wadau wanasema akaunti ya Kim Kardashian nayo inacheka kwa sana.
Je na wewe unatamani kujaribu gemu hili? Bofya kulingana na aina ya simu/tableti unatumia -> Android | iOS
No Comment! Be the first one.